Usinipunje, Nisikupunje, Tusipunjane- Kenani Kihongosi

Usinipunje, Nisikupunje, Tusipunjane- Kenani Kihongosi

kevylameck

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
18
Reaction score
19
Leo Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Kenani Kihongosi alikuwa Mkoani Geita kwenye muendelezo wa kampeni ya Sensa na Vijana.

Kampeni hiyo ilifunguliwa Mjini Dar es salaam kwa kauli ya kufanyika nchi nzima na sasa imetia nanga kwenye mikoa ya Kanda ya ziwa.

Maudhui na muktadha wa kampeni hii ni kuhamasisha vijana kujiandaa na kujitokeza kwa wingi Jumanne ya August 23 ili kushiriki kwenye zoezi la kitaifa na SENSA.

Katikati ya mabango kadhaa yaliyokuwepo uwanjani wakati Katibu Mkuu wa UVCCM Kenani Kihongosi anahutubia, nilipenda bango moja lililokuwa limeshikiliwa juu muda wote.

Bango hilo lilikuwa linasomeka hivi:

"Sensa ya Watu na Makazi"
- USINIPUNJE,
- NISIKUPUNJE,
- TUSIPUNJANE.
"Ujanja kuhesabiwa"

Bango hili nimelipenda kwasababu lilibeba maana nzima ya kile ambacho Katibu Mkuu wa UVCCM na Mh. Rais wetu Mama Samia wanachokizungumza kila wakati.

Ni muhimu mimi na wewe kushiriki kwenye Sensa kwasababu Sensa ndiyo inayotusaidia kwenye maana halisi ya kilichoandikwa kwenye bango nililoliona uwanjani.

Sensa itaisaidia serikali kufahamu idadi yetu, Kujua tulipo, jinsia zetu, hali zetu za kiuchumi pamoja na rika zetu na hali zetu za Kielimu.

Matokeo ya Sensa pia yanaisaidia serikali kufahamu hali ya uhamiaji, kwa maana ya kufahamu waliohamia nchini mwetu na wale wahamiaji wa kutoka vijijini kuja mijini au kutoka mijini kwenda vijijini.

Baada ya kufahamu haya ndipo'sa serikali sasa inapokuja na mipango halisia,sera zinazojibu changamoto halisi za kijamii sambamba na kujipima kwake kwa namna inavyotutumikia kisera na katika kutuletea raia wake maendeleo.

Sasa kwanini USINIPUNJE, NISIKUPUNJE,TUSIPUNJANE?

Ukweli ni kuwa kupitia matokeo ya sensa ndipo pia serikali inapokuwa na bajeti halisi, mpango mzuri wa ugawaji rasilimali za nchi kwa usawa sambamba na kufahamu mahitaji yetu halisi kulingana na jinsi zetu, rika zetu na idadi yetu kando ya taarifa nyingine muhimu watakazokusanya.

Hapa ndipo serikali itakapofahamu idadi ya watoto na mahitaji ya shule na waalimu wanaohitajika,watoto wasiokuwa shuleni na mahitaji mengine hitajika.

Serikali itafahamu idadi yetu na wingi wa hospitali zilizopo na zinazohitajika, vitendea kazi na wahudumu wanaohitajika kutokana na idadi ya watu katika eneo fulani.

Serikali pia itafahamu wingi na idadi ya watu wa makundi maalumu kwa maana ya watu wenye ulemavu, wazee na hali ya utegemezi waliyonayo na changamoto za kijamii wanazopitia na namna ya kuweza kuwasaidia.

Serikali pia itafahamu wingi na idadi yetu sisi vijana, hali yetu ya kiuchumi, shughuli tunazozifanya nk.

Majibu yake pia yatatoa taswira ya hali halisi ya tatizo la ajira nchini Tanzania na hivyo kuisadia serikali katika kutafuta masuluhisho yake.

Sasa napokosekana mmoja wapo ambaye hatahesabiwa maana yake ni kuwa ATATUPUNJA pale serikalini itakapokwenda kuandaa bajeti, sera, mipango na mikakati yake huku ikifahamu kuwa tupo 200 baada ya Sensa kumbe uhalisi ni kuwa tupo zaidi ya 250.

Utatupunja ama tutapunjana kutokana na uhalisia kuwa serikali inazitaka zaidi takwimu zetu ili kufahamu wapi wafanye nini na kwa watu wangapi hasa.

Utatupunja kwasababu serikalini pia itashindwa kujua Wafanye nini kwa namna ipi, wapi na kutokana na idadi ipi ya wahitaji? wapi wajenge hospitali? wapi waongeze shule au vyuo,vitendea kazi na hata miundombinu mingine muhimu.

Tutapunjana pia kwasababu serikali itakosa takwimu sahihi na kujua kwa usahihi ni namna gani washughulikie changamoto nyingine za kijamii kama tatizo la ajira lililopo, changamoto za wazee na wenye ulemavu, changamoto za vijana na wanawake na mengineyo.

Shime vijana! tujitokeze kuhesabiwa. Ni muhimu kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi ili Serikali itutambue na itujumuishe kwa umoja wetu kwenye sera, mipango na maamuzi wanayoyafanya kila siku.
48F5E332-5D4A-482B-9241-3616F4C31F66.jpeg
 
Na vyama vingine waunge mkono hizi kampeni nimezipenda.

Sasa CDM, CUF ,ACT nk wafanye hivi hivi itapendeza sana.

Au mnasemaje?
 
Baada ya watu kuhesabiwa nahisi sahv tanzania watu watafika mln 100

Ova
 
Katiba mpya italeta uwiano sawa kisiasa hata WANANCHI hawatoisusa serikali iliyopo madarakani kwakuwa waliichagua wao wenyewe kuliko uchafuzi huu uliopo sasa!!

Uwiano wa kisiasa itasaidia wananchi kushiriki kwenye kampeni za kitaifa KWA pamoja kuliko Sasa ambapo mazoezi ya kitaifa yanahamasishwa na na chama Tawala pekee tena uvccm badala kuwa na hamasa kitaifa KWA faida ya WOTE!

Narudia tena soma hapo paragraph ya Mwisho!!


"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Chadema amkeni... Mnalala Sana hadi mnaanza kutuboa wafuasi wenu. Naanza kupata wasiwasi na Mbowe. Kutwa kukutana viongozi wake serikali lkn hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom