Usiogope unaweza kujenga na kumiliki kituo cha kujaza mafuta ya vyombo vya moto vijijini cha gharama nafuu

Ili uwekezaji ulipe inatakiwa upate sehemu ambayo kuna mzunguko mkubwa wa magari hasa sehemu za mijini au wilayani huko vijijini ni kuchoma pesa unless uwe unalenga faida ya sh 500 kama wanavyofanya wale wanaouza kwenye vichupa vya lita.
 
Inategemea jinsi EWURA na makampuni walivyopanga. Mfano chukua mfano huu wa mwezi may ilikua ni hii:

161.18 Tsh per lita kwa petroli

160.7 Tsh per lita kwa dizeli

159.36 Tsh per lita kwa mafuta ya taa
Inakuwaje makampuni ya mafuta yanakuwa tajiri wakati faida kwa lita ni ndogo sana?
Mfano ili kampuni iweze pata milioni 161, yatakiwa uza lita milioni 1

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
mtoa mada bado hujaongezea kitu je ukiwa huko vijijini hayo mafuta unayafuata mwenyewe ? na je unaletewa na magari ya mafuta kwa wenye magari je garama za kukodi gari kuyatoa unapoyanunua mpaka unafikisha kwenye kituo chako ni ngap

kumbuka ukiwa kijiji sana pia garama ya kufikisha kwenye kituo chako ni kubwaa kuliko wa mjini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante sana kwa kukumbushia jambo muhimu.
Mzigo unaweza kusafirisha kwa Lori la kukodi kutoka bandarini mpaka unapouzia.
Kuhusu gharama za usafiri usijali kwani bei ya kuuzia kwenye kituo chako, EWURA wanaangalia umbali uliopo toka uliipoyatoa mafuta mpaka hapo unapoyauzia.
 
Inategemea na kijiji kilipo. Kijiji cha Pwani ni rahisi kuliko Kigoma mjini
 
Watanzania wengi wangekuwa na moyo kama wako hakika nchi ingekuwa mbali sana sana.
Nakukuhakikishia yote haya uliyo share nasi Kuna watu watachukia sana sana Maana mtindo wetu waswahili endapo Kuna fursa nzuri unajua na huna uwezo upo tayari fursa hiyo ipotee kuliko kushare na mtu mwingine ambaye atathubutu.

Watu wanatumia fursa hii uliyotufundisha kimya kimya bila kumshirikisha mwingine... Wakati tanzania ina vijiji zaidi ya 12,000/=
Ni ve sana sana kushare fursa mbali mbali bila kinyongo wala hofu. Sio lazima uliomsaidia wazo jema akifanikiwa aje akushukuru no. Mwenyezi Mungu atakuletea na fursa nzuri unayoiweza na itakayokutoa kupitia hata mtu usiyemtarajia.

Ubarikiwe sana sana mkuu.
 
Ahsante sana boss kwa ujumbe uliojaa maarifa, karibu sana
 
Inakuwaje makampuni ya mafuta yanakuwa tajiri wakati faida kwa lita ni ndogo sana?
Mfano ili kampuni iweze pata milioni 161, yatakiwa uza lita milioni 1

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kwa mwezi Tanzania nzima ina consume 400 million litres za mafuta...pia ukichukua 161,000,000÷2969 = 54,227 Litres...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…