Usiombe mabaya yatakukuta

Usiombe mabaya yatakukuta

Bwana Bongo

Senior Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
146
Reaction score
212
Usiombe mabaya yatakukuta

porojo za bongo

15-02-2011 ilikuwa jumanne tulivu, tukiwa uwani tukipiga stori za hapa na pale, nawakumbuka baadhi ya watu wachache tulio kaa pale uwani, dada g,dada asha, mrs siliver michael, siliver michael , mama g au mrs benny na mzee dondola alikaa kwa mbali kidogo akivuta embassy yake

Baada ya kushiba ugali, siliver akawa anapiga nyimbo zake za kijaruo na kutafsiri, na kwa vile alikuwa mwalimu ni mzuri kueleza mambo, basi tulimtegea sikio kwa makini
kuyasikiliza malalamiko ya mwanamuziki yule wakijaruo, nanukuu tafsiri ya siliver kwa uchache

"mapenzi si vita,hatushikiani bunduki,kilio changu juu yako, nasauti nayo kuimbia, inaweza kukauka, vyote hivyo vinaweza kuisha, nini utapenda nikupe, najua pesa ndo kila kitu, nashanga kwamba niweza kuwa na pesa, kisha nisikupate, umefungua moyo wangu, au unataka nikwambie kasoro yako, kasoro yako ni kutokuwa na kasoro"

Wote tuliangua kicheko, eboo kasoro ni kutokuwa na kasoro kweli wanaume tutakapo chetu atushindwi , gafla tukaangukia katika habari za mabomu ya mbagala, baada ya kusikia taili la gari nimebasti, japo nilikuwa mdogo lakini nilianza kuadithia kuhusu jinsi tulivyo fungiwa darasani kisha mama mmoja mnene, mwenye watoto mapacha hassani na husseni, alivyo mkwida mwalimu ampe funguo za darasa walilosoma watoto wake ambalo na mimi nilikuwemo, dada g na dada asha wakaleta mzaha na kudhiaki kwamba huyo mama alikuwa muoga, kwa vile wao awakujua chungu na tamu ya mabomu ya mbagala, mama g akasisitiza kwamba wasionge hivyo, sababu hata yeye alipoteza fahamu na ukweli siku hiyo roho yake ilikalibia kutoka

Dada g akasema " kwani yana liaje puuuu au mbuuuu" mimi natamani kuyasikia kweli" dada asha akaogezea nakuangua kicheko, hawakuwa kipindi cha mlipuko wa mabomu ya mbagala hivyo waliposikia stori za kubeba paka na kuacha watoto wao, wakazidi kucheka na kuzani vilikuwa vichekesho

Stori zikaisha kila mmoja akaingia mlango wake asubuhi ikatukuta tukiwa salama kisha kila mmoja akaingia katika mizunguko yake, tulipokutana tena jioni na kwa bahati nzuri au niseme mbaya sikuiyo umeme ulikatika hivyo tuka jikusanya pale uwani kama desturi yetu ya kila siku, vitu vikaanza kujibu

wakalia kwa kusaga meno

ilikuwa jumatano ya tarehe 16-02-2011 mabomu yakalipuka usiku kambi ya gongo la mboto

usiombe mabaya yatakukuta!

#Bwanabongo
 
Back
Top Bottom