Usiombe uumwe USA

Natalia

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2011
Posts
4,324
Reaction score
1,892
Kuna mdada mmoja mkenya aliumwa 2 weeks saa hizi nyumba hajalipa gari umeme na maji an simu .na kazi Hana Leo kuna kikao cha kumchangia.maisha gani hayo siheri Arudi Kenya tu .unaumwa week 2 tu unakutwa na drama lote hilo.kuishi paycheck to paycheck no heri urudi bongo
 
Sisi huku tuna afya tele tunavimbiwa, hospitali kibao unaandikiwa dawa pharmacy kila kona. Daladala tuna mpaka treni sikuizi, bado ya ndege kwenda moshi mbeya mwanza kila mahali magufuli yupo bwana na mwakyembe wataleta kwanini mnapata shida huko si mrudi huku simu sio lazima uweke hela unaweza kuwa una beep tuu unapigiwa nyie mpaka mlipe! Kila mahali hapa ukibanwa mkojo unakojoa njooni huku waachieni mashida yao!
Maboga, mihogo, mahindi. Maharage mabichi weee njooni. Kuna ng'ombe wa kupeleka kwa dume kule home njooni tusaidiane
Njooni bwn msitesekee kwa watu kwani huko mnafanya nini. Wazee wete majukumu yamewazidi huku magogoni mje kuwasaidia.
 
huku simu sio lazima uweke hela unaweza kuwa una beep tuu unapigiwa nyie mpaka mlipe! Kila mahali hapa ukibanwa mkojo unakojoa njooni huku waachieni mashida yao!.

Hii ni kali kuliko zote, Looh!
 
Haweki akiba, bora arudi nyumbani. America matatizo sana
 
Kuishi uropa siyo kuukata hasa kwa wale waliokwenda kule bila mipangilio ya uhakika. Heri warejee makwao wakapige nguna maana hakuna kitu kinachouma kuona watu wanavyodhalilika hasa akifa mmojawapo kwa kuchangishana.
 
Ila hizo huduma zake! Bila kutoa kitu kidogo hupati ya maana.

NN si afadhali utoe kitu kidogo utibiwe kuliko kuishi maisha ya mashaka kama hayo? Mtu kama husomi na wala huna kazi ya maana ya nini kung'ang'ania huko?
 
Maisha ya USA sio rahisi kama wengi wetu tunavofikiria unaeza pata kazi ukalipwa $15 kwa saa kwa kwetu ukaona ni nyingi sana kwa masaa 40 lakini matumizi uwe na utaratibu vyengine itakula kwako
Wanaopata shida zaidi ni wale wasio na karatasi unashindwa kudai masilahi yako kwani ukiumwa kama una karatasi basi kuna short and long time disability ambayo kazini watakulipa mshahara wako kama kawaida ila utakatwa baada ya muda na makato ni kidogo sana kila paycheck
Mwisho kama huna karatasi basi jaribu kishi watu watatu au wanne ili kusaidiana kwenye gharama
 
Ni mambo ya kawaida tu katika maisha hata Bongo mambo unaweza kuishia ukakosa pesa ya kwenda hosp, na hata kulipa pango la nyumba, mi nampa pole na najua hata yeye atakuwa amepata funzo na hata kama kuna kikao cha kumsaidia mtu, C lazima mmtangaze
 
NN si afadhali utoe kitu kidogo utibiwe kuliko kuishi maisha ya mashaka kama hayo? Mtu kama husomi na wala huna kazi ya maana ya nini kung'ang'ania huko?

wanang'ang'ania kuona maghorofa....majumbani wakisimulia BT yupo marekani full ujiko
 
Mtu kama husomi na wala huna kazi ya maana ya nini kung'ang'ania huko?
Kama husomi na huna kazi ya maana unang'ang'ania nje kwa sababu Bongo kama huna elimu na huna kazi nzuri maana yake unasukuma mkokoteni Tabata Dampo... bora kulea wazee mbele huko
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…