Usipange Kuhusu Maisha, bali Tumia fursa Katika Maisha.

Usipange Kuhusu Maisha, bali Tumia fursa Katika Maisha.

masandare

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
671
Reaction score
574
Habari wanajamvi!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kamwe usijepanga kuhusu maisha yako , bali badala yake yakupasa kutumia fursa unayokutana nayo katika maisha. Yawezekana ukawa unakinzana na unachokiamini ila ukinisoma na kuyapa nafasi haya maneno tutakuwa pamoja.

Nnaposema usiyapange maisha , simaanishi eti usiwe ndoto , au usitamani vitu fulani. Ukitaka kujua validity ya nnachokisema anza kujiangalia wewe mwenyewe hapo ulipo na maisha uliyonayo ni kutokana na ulivyoyapanga au ni kulingana tu na mambo yalivyokuwa?

Hivyo basi iwe kuhusu kuoa, kuolewa, kujenga, kusafiri, nk. Yote yanaingia. Kwa nadharia hii nnayoiwasilisha nyuma yake ndipo zilipozaliwa misemo na methali nyingi kama Usimtukane mkunga uzazi ungalipo, Usimtukane mamba kabla hujavuka mto, Usilolijua usiku wa giza, Nk.
Maneno yangu hayamaanisha eti kabla hujaliendea eti usiwe na mikakati ktk kulifanikisha.
Karibuni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom