Usipokuwa na familia, ndugu na jamii kwa ujumla hukuchukulia kama mtu asiye na majukumu

Ben-adam

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
1,043
Reaction score
2,309
Katika jamii yetu, kuna mtazamo wa kuona mtu asiye na familia kama mtu "asiye na majukumu makubwa." Kwa sababu ya mawazo haya, mara nyingi watu wasio na familia hupokea maombi ya msaada mara kwa mara kutoka kwa ndugu, jamaa, au marafiki. Wakati mwingine, hili linaweza kumchosha mtu, hasa anapohisi kuwa msaada anaotoa unachukuliwa kama jukumu lake kwa sababu hana familia.

Ni wakati mwafaka wa kubadilisha mitazamo hii. Mtu anaweza kuwa na majukumu makubwa na kuwa na mipango ya maisha hata kama hana mke au watoto, na jamii inapaswa kujifunza kuheshimu nafasi hiyo.

Katika mtazamo wa wengi, mtu asiye na familia hudhaniwa kuwa na muda mwingi na uwezo wa kifedha kwa sababu hana watu wa kuwatunza moja kwa moja. Huu ni upotoshaji, kwani kila mtu ana mipango, malengo, na wajibu wa kibinafsi, na kutokuwa na familia haimaanishi kuwa mtu hana majukumu mengine.

Ni muhimu kuwaelewesha wengine kwamba majukumu siyo tu yale yanayohusu familia, bali yanaweza pia kuwa katika mipango ya mtu binafsi, majukumu kwa wazazi au ndugu wengine, na hata dhamira za kimaendeleo. Kwa mfano, baadhi ya watu wanaweza kuwa na mipango ya kuwekeza katika biashara, kujiendeleza kitaaluma, au kutoa mchango katika jamii. Majukumu haya pia yanahitaji muda, rasilimali, na kujitolea.

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa kusaidiana, hasa miongoni mwa familia na marafiki. Hata hivyo, ni vyema kuwa na uwiano katika msaada tunaotoa kwa wengine na pia kujali mipaka ya wengine. Sio kila ombi la msaada linafaa kutegemewa kwa mtu mmoja kwa sababu tu anaonekana "hana majukumu ya kifamilia." Mtu asiye na familia pia ana malengo na mipango yake.

Kwa mtu mwenye mipango ya kibinafsi, kazi, na ndoto, kutokuwa na familia haimaanishi kwamba hana majukumu muhimu. Jamii inahitaji kuelewa kuwa uwajibikaji siyo tu kwa familia, bali unajumuisha mipango na malengo ya kibinafsi ambayo yanahitaji kujitolea na kujali.

Kama mtu asiye na familia, inaweza kuwa muhimu kuweka mipaka ya wazi juu ya msaada unaoweza kutoa. Hii siyo tu kwa ajili yako, bali pia kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondokana na mtazamo wa kuwa msaada ni wajibu wa watu fulani tu.

Kuwajibika si Hali ya Ndoa au Familia Pekee
 
Kwaniiiii, ni nini kinakufanya usiwe na familia? na ni nini kinakufanya usaidie familia za wengine? Je kwenye huo msaada katika familia isiyo yako unasimama nao 100% au ukiwarushia kilo ya maharagwe unatangazi umesaidia. Sikia, inawezekana kuna shida kwenye familia ulikotoka lakini usiogope, kuwa na familia yako ni kitu kizuri sana na utaenjoy mna HASA ukijua jinsi ya kujenga familia yako.
Ni kweli mtu asiye na familia ataonekana hana majukumu na hajitambui... na ndivyo ilivyo.
Kabla hujaamua kuwa nayo au kutokuwa nayo tafuta hasara na faida zake!
 
kumsaidia mtu au kutokumsaidia ni uamuzi wangu binafsi, iwe nina familia au sina. hakuna wa kunilazimisha, kila mtu na aishi maisha yake anayoona yana mfaa.
 
Kwa maisha haya haya ya hii dunia ya kisasa,ukiyafanya huku unawaza watu wengine wanasemaje kuhusu wewe hufiki mahali,maana utataka wao wakuamulie kila kitu,utajikuta umeingia kwenye gereza la ndoa usiyoitarajia kwa sababu tu unawaza watu wanakufikiriaje,Bro hayo ni maisha yako,usukani wa gari unao wewe,hivyo elekeza gari unakotaka.
 
Kwaniiiii, ni nini kinakufanya usiwe na familia? na ni nini kinakufanya usaidie familia za wengine? Je kwenye huo msaada katika familia isiyo yako unasimama nao 100% au ukiwarushia kilo ya maharagwe unatangazi umesaidia. Sikia, inawezekana kuna shida kwenye familia ulikotoka lakini usiogope, kuwa na familia yako ni kitu kizuri sana na utaenjoy mna HASA ukijua jinsi ya kujenga familia yako.
Ni kweli mtu asiye na familia ataonekana hana majukumu na hajitambui... na ndivyo ilivyo.
Kabla hujaamua kuwa nayo au kutokuwa nayo tafuta hasara na faida zake!
Ratan tata, Isaac Newton, Keanu Reeves, Da Vinci, hawa jamaa ni wajinga sana na hawakuwahi kujitambua!
 
Unakuta una majukumu makubwa kuwasomesh ndugu zako hadi kuanzisha familia ni unaogopa.
 
Kwa maisha haya haya ya hii dunia ya kisasa,ukiyafanya huku unawaza watu wengine wanasemaje kuhusu wewe hufiki mahali,maana utataka wao wakuamulie kila kitu,utajikuta umeingia kwenye gereza la ndoa usiyoitarajia kwa sababu tu unawaza watu wanakufikiriaje,Bro hayo ni maisha yako,usukani wa gari unao wewe,hivyo elekeza gari unakotaka.
Kabisa mkuu ile pressure ya umeoa utaoa lin unkuta umekurupuka kuoa ukapata mtu ambae si sahihi unanza kuteseka.
 
  • Thanks
Reactions: M45
Unakuta una majukumu makubwa kuwasomesh ndugu zako hadi kuanzisha familia ni unaogopa.
USIOGOPE.
Unapoogopa na kubaki peke yako ndipo jamii inapoona huna majukumu na wanaamua kukupa majukumu kwa sababu kila binadamu anatakiwa kuwajibika hapa duniani ndio maana kama huna familia unawajibishwa taka usitake na maneno juu.... na masimango kibao.. na dharau kutoka kwa hao wenye familia uliowasaidia.
 
Shida ni kuwaambia kiwango cha hela zako.
😀😀😀 Watajua tu hata usipowaambia. Na ikitokea huna hela pia watakupa majukumu hata ya kulinda nyumba zao wakisafiri kwenda msibani au harusini .... maana upo upo tuuuuu hakuna atakayejali eti umeamua kuwa peke yako bila familia basi wakuache tuuuu.....
 
Hahaha, sasa hapo itategemea na vile ulivyo.
 
Kabisa mkuu ile pressure ya umeoa utaoa lin unkuta umekurupuka kuoa ukapata mtu ambae si sahihi unanza kuteseka.
Msije Mkasema hatujawaambia, kosea vyote ila usikosde kuoa au kuolewa utajuta maisha yako yote.

Wenye ndoa zetu tunatamani kuwa single kuliko kuendelea na hili gereza la kujitakia la ndoa.

Waswahili huwa hatuambiani ukweli, shida anazopata mtu anataka ña wengine wapate shida kama zake.

Jiulizeni kwa nini watu wana ndoa zao na mpo nao club mpaka majogoo?
 
Wengine wanandoa ila tunagombea mademu kama kawaida.
 
Back
Top Bottom