Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

"Hivi mtu aliyepoteza fahamu anaweza kuielezea hali ya kupoteza fahamu ikoje? yani wakati amepoteza fahamu kuna ambacho anaweza kukieleza ambacho kilikuwa kikiendelea wakati hana fahamu?"

Kiukweli, hawezi. Kwake, hakukuwa na hali yoyote ile, kimsingi hakukuwa na chochote kwake hadi atakapopata fahamu na kuelezwa hali ilivyokuwa. Sasa, hebu fikiria mtu huyu alipoteza uwepo kabisa, kwake ni kipi hasa ambacho kingekuwepo?
 
Mimi na wewe tupo kwa kuwa tupo. Sasa hivi mimi nisipokuwepo, wewe haupo kabisa na wala hukuwahi kutokea, labda siku nikiwepo tena, jambo ambalo si rahisi. Kwa hiyo, mimi nisipokuwepo, wewe hukuwahi kuwepo na hutakaa kuwepo.
Mkuu mie naona unarudia yaleyale tu sioni kipya,naona unalazimisha tu.
 
Yani unasema kabisa kuwa kuna wakati hukuwepo na huna kumbukumbu yeyote ila hapohapo unaeleza hali ya wakati huo wakati ushasema kuwa hukuwa na kumbukumbu!!
 
Ndugu, wewe leo usipokuwepo kuna namna unaweza kusema ama kuwa na ufahamu wa kuwa maisha yanaendelea au yalishakoma?
Na ndiyo maana nakushangaa ufahamu wa kwamba hakukuwa na chochote wakati wewe haupo umeupata wapi?
Maana ni sawa na kusema asiyekuwepo ana ufahamu kuwa maisha hayaendelei kwa maana hakuna kitu.
 
Itakuwa haujafanikiwa kutoka upande wa pili wa bomba hivyo huwezi kujua kuna vitu gani na wala huwezi kujua kuwa hakuna kitu,na yote ni kwa sababu ya kukosa fursa ya kutokea upande wa pili.
 
Sasa utasemaje tuna uzowefu wa kutokuwepo? sasa kama mtu aliyepoteza fahamu tu hana chochote anachoweza kuelezea kama uzowefu wake katika hali ya kupitia upotevu wa fahamu,je vp asiyekuwepo awe na uzowefu?

Kama aliyezimia anatuhitaji sie kumuelezea yaliyokuwa yakiendelea pindi hana fahamu,hivyo ni sawa na asiyekuwepo.
 
Yani unasema kabisa kuwa kuna wakati hukuwepo na huna kumbukumbu yeyote ila hapohapo unaeleza hali ya wakati huo wakati ushasema kuwa hukuwa na kumbukumbu!!

Ninaweza kusema hivyo kwa kuwa nipo mkuu. Yaani kwa kuwa nipo, sina ufahamu wowote wa kabla ya kuwepo kwa maana ya kwamba hakukuwa na maisha. Uliuliza pia kuwepo kunaanza wakati gani. Kuwepo ninapomaanisha mimi ni maisha baada ya kuzaliwa.
 

Ndio, tunaweza kusema hakuwepo na pengine huu ni mfano mzuri wa kutokuwepo, uzuri ni kuwa mtu huyu anapotea kwa muda mfupi. Katika kipindi hiki cha kupotea, kwake karibu kila kitu hakikuwepo, hata waliokuwa wamemzunguka. Ikiwa una amini kuwa aliyepotea kwa muda hana anachoweza kukielezea, je inakuwaje kwa mtu asiyekuwepo kabisa? Mimi nipo, na kuna wakati sikuwepo, sawa ndugu? Kutokuwepo tayari ni uzoefu. Katika hali ya kutokuwepo, sina kumbukumbu yoyote ya chochote katika hali hiyo. Kwa kuwa siwezi kusema chochote kuhusu kutokuwepo, siwezi kusema kuwa kuna watu, ama nyumba ama vitu kwenye maisha hayo. kwa hiyo, hakuna chochote kwenye maisha ya kutokuwepo.
 
Itakuwa haujafanikiwa kutoka upande wa pili wa bomba hivyo huwezi kujua kuna vitu gani na wala huwezi kujua kuwa hakuna kitu,na yote ni kwa sababu ya kukosa fursa ya kutokea upande wa pili.

Ndivyo hivyo hivyo mkuu, unapokosa fursa ya kuwepo, hali ndio inakuwa hivyo, kamwe hutojua upande wa pili (wa uwepo) ueleze nini. Kwanza tu, baada ya kutokuwepo, unakosa hata ufahamu wa kujua ikiwa kuna upande wa pili, achana na vitu vilivyopo upande wa pili. Kwako, kimsingi, katika hali kama hii, hakuna chochote, hakukuwahi kuwa na chochote, hata hukuwahi kupita kwenye bomba lenye giza. Hata wewe mwenyewe hukuwahi kuwepo, mara tu baada ya kupoteza uwepo.
 
Yani unasema kabisa kuwa kuna wakati hukuwepo na huna kumbukumbu yeyote ila hapohapo unaeleza hali ya wakati huo wakati ushasema kuwa hukuwa na kumbukumbu!!

Nielewe vizuri mkuu. Ni sawa na mtu akupeleke mahali ambapo hujawahi kufika akiwa amekufunga macho. amekufikisha mahali hapo, akakwambia hapa tupo Arusha. Baadae ukarudi Dar, akakufungua macho. Kisha akaja mtu akawa anakuuliza kuhusu mwonekano na uzuri wa Arusha. Utamweleza nini? Una kumbukumbu ya kufika Arusha, lakini huna lolote la kusema kuhusu Arusha.

Ninatambua kuna wakati sikuwepo, na utambuzi huu unawezekana tu kwa kuwa sasa nipo. Ila, katika kutokuwepo, sina kumbukumbu yoyote ya kilichojiri. Kama nilijenga, nilioa, niliacha watu na vitu, kuna maisha. Hilo sina kabisa. Kwa hiyo, kwangu, hakuna chochote kwenye maisha ya kabla ya kuwepo. Hakuna lolote ninaloweza kulisemea ama kulishuhudia. Sikuwepo (uzoefu unaotokana na kuwepo) sasa nipo (uzoefu) na kuna siku sitakuwepo (hili nalo ni kutoka kwenye uzoefu wa kuwepo). Ila, huwezi kusema hata siku ambayo hutakuwepo, utakuwa na uzoefu wa kuwa kuna uwepo. Hili halipo. Uzoefu wa kuwepo unaonesha hakuna namna uligundua uwepo kabla ya kuwepo.
 
Ninaweza kusema hivyo kwa kuwa nipo mkuu. Yaani kwa kuwa nipo, sina ufahamu wowote wa kabla ya kuwepo kwa maana ya kwamba hakukuwa na maisha. Uliuliza pia kuwepo kunaanza wakati gani. Kuwepo ninapomaanisha mimi ni maisha baada ya kuzaliwa.
Mkuu uwepo wetu umeanzia kwenye matumbo ya mama zetu na si baada ya kuzaliwa. Na hakuna kati yetu mwenye kuyakumbuka hayo maisha ya tumboni yalikuaje.

Je,unataka kusema hakukuwa na kitu wakati wa kabla ya kuzaliwa kwa kuwa hatuna ufahamu wowote kabla ya kuzaliwa?
 
Na ndiyo maana nakushangaa ufahamu wa kwamba hakukuwa na chochote wakati wewe haupo umeupata wapi?
Maana ni sawa na kusema asiyekuwepo ana ufahamu kuwa maisha hayaendelei kwa maana hakuna kitu.

Ndugu, ninasema hakukuwa na chochote kwa kuwa sasa nipo. Uzoefu wa kuwepo unanipa uwezo wa kufahamu kuwa sikuwepo na ninapojaribu kuwaza kuhusu maisha ya kutokuwepo, hakuna lolote ninaloweza kusema wala kukumbuka. Kama una nguvu ya kusema kuwa kuna uwepo katika kutokuwepo, basi tumia uzoefu wa kuwepo kueleza mambo yaliyopo kwenye kutokuwepo.

Labda tusaidiane pia kuwaza katika hili. Je ambacho hakijavumbuliwa kipo? Unaweza kukitaja, kipo wapi, kina muonekano gani? Kina miguu, kinaongea, si hai, ni hai, kinaitwaje n.k. Hivi, tunakosea tunaposema hakuna dawa ya ukimwi au ya kansa? Au itakuwepo wakati ambao itakapokuwepo (vumbuliwa?).
 
Ninapigilia msumari hapo mkuu, hakukuwa na chochote. Yawezekana unaweza kuuliza, sasa umezaliwaje? Fikiria kuwa usingezaliwa (kuwepo) kama ungekaa kujua kuwa kuna wazazi. Ili uone, unahitaji mwanga mkuu (macho yapo lakini yasingekuwa na maana yoyote(kwa namna yalivyo) bila mwanga, na ili mwanga utumike kwako, lazima uwepo.
 
Huwezi kusema mtu aliyepoteza fahamu kwake kila kitu hakipo,wakati tukio lenyewe linaitwa "kupoteza fahamu" na ndiyo maana akizinduka atahitaji watu wamueleze yale yaliyokuwa yametokea pindi akiwa hana fahamu.

Hivyo utaona hapo tatizo ni ufahamu na si kwamba hakuna kilichokuwepo wakati yeye hana fahamu,hanalichokiexperience kwa kuwa hakuwa na fahamu.

Sasa hapo hoja ya kwamba hakukuwa na chochote sijui unaiwekea wapi.
 
Hii hili jibu la hakukuwa na chochote linapatikana vp na wakati hata hukuwepo? hukuwepo hivyo hakuna namna ya kutambua kilichopo au kisichokuwepo.
 
Arusha kuna baridi mkuu hivyo utahisi hiyo baridi na ukirudishwa lazima uhisi hali Dar lazima uhisi hali ya hewa tofauti.

Hivyo unaweza usiiyone Arusha ila unacho ulicho experience na utaweza kuelezea,ni tofauti na kwamba haupo unafikiri utaeleza nini?
 
Kwahiyo vipofu wote hawapo?

Labda nikuulize hivi baada ya kuzaliwa ndiyo unakuwa hai au uhai unaanzia kabla ya kuzaliwa?
 
Sema kuwa usipokuwepo, vilipo vilivyopo na vilivyokuwepo wakati wewe haupo, haviwezi kuwepo ulipo.
 
Hii hili jibu la hakukuwa na chochote linapatikana vp na wakati hata hukuwepo? hukuwepo hivyo hakuna namna ya kutambua kilichopo au kisichokuwepo.

Kama siwezi kutambua kilichopo au kisichokuwepo na sitaweza kutambua milele, tafsiri yake ni nini mkuu? Siyo kwamba hakuna chochote?
 
Ndio hivyo mkuu na ninafurahi kuwa unatambua umuhimu wa kuwepo. Usipokuwepo, huwezi kueleza chochote na kama utashindwa kueleza chochote milele, ni kusema hakuna chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…