Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,057
- 7,611
Jana nimemwona waziri fulani kwenye tv anaongea kuhusu kisukari na hari inavyozidi kuwa mbaya ukizingatia na gharama ya matibabu lakini kidogo wakati anataka kuongea juu ya sababu ghafla akasita akazuga anaongelea idadi ya wagonjwa,tena baadae nikaona ile ya saratani ya shingo ya kizazi wakaoneshwa wanawake wengi wanavyoitikia kwenda kupima pale Tabora,nikajiuliza moyoni,inakuwaje wanahamasishwa kuchukua vipimo na matibabu na si kuelezwa ni kwa jinsi gani hasa ama ni kwanini mpaka maradhi haya yanawapata akina mama?
Nikaunganisha yote mawili nikaona bora niulize,serikali na wauguzi mmeona ni bora tiba kuliko kinga? inakuweje hamkazii sana elimu ya kujikinga na haya magonjwa badala yake mnapromote zaidi matibabu,hii si tiba kuliko kukinga?