Ndugu wanajukwaa kama kichwa cha habari kinavyosomeka.
Ninaomba kuuliza swali: je, tuendelee na utaratibu huu wa mikataba kuwa siri au tubadilishe utaratibu mikataba iwe wazi ili kila mtu ajue mashariti ya hiyo mikataba kama yana faida au lah?
Nimeuliza swali hili kutokana na mjadala unaoendelea kuhusu kuhuisha mradi wa bandari ya Bagamoyo au huo mradi ufe kabisa kutokana na masharti yake kuwa ya kinyonyaji kama tulivyoambiwa.
Binafsi nashindwa kuwa na upande katika hili maana huo mkataba sijauona zaidi tu ya kuambiwa na shujaa kuwa mashariti ya mkataba ni kichaa.
Lakini kabla ya shujaa, huo mradi ulipotangazwa mwanzoni ulipigiwa promo sana na Mtangulizi wake akielezea faida lukuki ambazo tungezipata kama nchi. Watu wengi walishangilia na kuona kama nchi yetu itakuwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Hatukuwahi kumsikia shujaa akiupinga kwa namna yoyote ile kabla hajawa Kocha Mkuu.
Alipoupata ukocha ndo aliamua kusitisha huo mradi kwa kutueleza mashariki ya mkataba namna yalivyo mabaya na ambayo kwakweli ukisikiliza ni mashariti mufilisi kabisa.
Hata hivyo baada ya shujaa kututoka huo mradi umeanza kupigiwa promo tena kitendo kinachotuacha wananchi njia panda.
Tunabaki njia panda ni kwasababu wananchi hatujapewa fursa ya kuiona hiyo mikataba physically ili tujionee wenyewe kilichoko ndani badala ya kusubiri kuambiwa tu na watawala wetu ambao kwa kiasi kikubwa sio wakweli (Mpaka hapo hatujui mkweli ni yupi kati ya aliyeuleta huo mradi na aliyeusitisha)
NB. Kama mnakumbuka wakati mradi gesi ya Mtwara unaanzishwa tuliambiwa huo mradi ukikamilika utakuwa ndio mwarobaini wa tatizo la umeme tulilonalo kama nchi.
Tuliambiwa kwamba gesi ni chanzo cha uhakika cha umeme tofauti na vyanzo vingine kama maji na mafuta.tuliambiwa vyanzo vya maji sio reliable maana muda wowote kunapotokea ukame au mafuriko basi chanzo hicho hakiwezi kuzalisha umeme kwa ufanisi na kwa kiwango kinachohitajika. Pia kuna suala la mabwawa kujaa matope hilo nalo ni tatizo kwa umeme wa maji lakini pia tuliambiwa hata gharama za uzalishaji ni kubwa. Hivyo tuliambiwa umeme wa gesi ndio mkombozi maana ni wa uhakika na gharama zake ni nafuu.
Mungu si Athumani mradi ukakamilika licha ya kuwa kuna watu walijaribu kuuzuia lakini cha moto walikiona.
Sasa tujiulize baada ya mradi kukamilika je tatizo la umeme tumeshalimaliza kama tulivyoambiwa? Je, gharama zake ni nafuu kiasi gani?
Je, kwa sifa zile walitudanganya au zinafanana na hali ya umeme iliyopo?
Nadhani kila mmoja wetu jibu analo.
Shujaa wetu alipoingia hajataka kujishughulisha kwa kiasi kikubwa na mradi huo kwa kile alichosema hauna manufaa ya maana ukilinganisha na stieglers gourge.
Yaani sasa umeme wa maji ndio unapigiwa promo kwa nguvu zote kwamba huu sasa ndio mkombozi wa tatizo letu la umeme. Kiwango kitakachozalishwa kitatosha na tutapata ziada ya kuuza nje. Pia tunaambiwa hata gharama za uzalishaji ni nafuu na hivyo bei kwa mraji itapungua sana.
Lakini pamoja na promo kubwa namna hiyo bado mikataba yake imeendelea kuwa siri ikiwemo ya standard gage.
Hata kama faida za mradi huo ni kubwa kiasi hicho tunachoambiwa je mashariti ya mikataba yakoje? Sio mashariti ya kutuumiza kama ilivyokuwa kwenye miradi mingine au kama tulivyoambiwa kwenye mradi wa bandari ya Bagamoyo.
Je, Watanzania ni kitu gani kinatufanya tuamini kwamba miradi ilioanzishwa na shujaa mikataba yake haina mashariti ya kinyonyaji kama ilivyo kwa miradi mingine?
Je, hatuoni sasa iko haja ya kudai kwa nguvu zetu zote uwazi wa hiyo mikataba tunayoingia kama nchi?
Je, hizo sababu tunazoambiwa kwamba mikataba inafanywa siri kwasababu investors tunaoingia nao mikataba hawaki mambo yao yawekwe wazi kwasababu za kibiashara na kiusalama.
Je kwa hapa tulipofikia hizo sababu bado zina mantiki?