RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara wa 27:
Ukaribu uliopitiliza kati ya Mwenza wako na marafiki zako ni hatari sana. Ukaribu wa marafiki zako kwa Mwenza wako ukipitiliza mambo huwa hivi.
1. Leo wanaitana "shemeji"
2. Kesho wataitana "shemu"
3. Keshokutwa wataitana "meji"
4. Mtondogoo wataitana "shemu darling"
5. Siku inayofuata wataitana "tunakulaga"
Kamwe usiruhusu ukaribu uliopitiliza kati ya Mwenza wako na marafiki zako (mashemeji zake). Wezi wengine huibuka kwa sababu ya mali iliyoachwa sehemu nyeupe. Hata kama nyumba yako ni imara hupaswi kuacha milango wazi, usimwache mwizi aibe mali yako kirahisi.
USIRUHUSU:
1. Usiruhusu Mwenza wako kusafiri mara kwa mara umbali mrefu na rafiki yako.
2. Usiruhusu Mwenza wako kwenda Lunch na rafiki yako mara kwa mara bila uwepo wako.
3. Usiruhusu mawasiliano ya karibu ya simu kati ya rafiki yako na mwenza wako (wanachati mpaka simu inakuwa ya moto).
4. Usiruhusu rafiki yako awe hakimu wa kudumu wa kusuluhisha kesi za wewe na Mwenza wako. Pia rafiki yako asiwe daktari wa kutibu upweke wake.
5. Usiruhusu Mwenza wako ajue kuwa kila unapokwama kifedha, sponsor wako mkubwa ni rafiki yako.
Je, ni kitu gani kingine kisiruhusiwe?
Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 1, 2024