Usisaidie masikini, acha wafe

Umaskini kwa tafsiri isiyo rasmi ni hali ya mtu kupungukiwa au kukosa kitu, au vitu, au mahitaji muhimu kwa maisha. Kimsingi, kuna aina mbili za Umaskini, MOSI, Umaskini wa mwili, ambao, Ni kupungukiwa kabisa uwezo wa kujikimu kwa mahitaji muhimu ya maisha, eg. Chakula, maji, afya, usalama, mavazi, makazi, pesa, nk. Umaskini huu hujulikana pia kama Umaskini wa Kipato. Umaskini huu ni mbaya mno na ni changamoto kubwa ktk kumtumika (kumwabudu) Mungu ipasavyo ktk Roho na Kweli pia. Ni vigumu mno kwa maskini kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Ni ngumu sana. Ndugu Robert kaelezea vya kutosha.
Kwa Wakristo tunaamini kisababishi au chanzo kikubwa cha Umaskini wa mwili ni Shetani-ibilisi. Na ndiyo maana Bwana Yesu Kristo alikuja kutusaidia tuushinde Umaskini wa mwili (2Wakorintho 8:9). Biblia inasema tena juu ya hili ktk kitabu cha 1Yohana 3:8; ... Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu (Yesu Kristo) alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Umaskini wa mwili, kwa hakika ni LAANA. Tuukatae na Tuupige vita kwa kufanya kazi kwa Bidii na Maarifa. PILI, ni Umaskini wa roho. Huu ni upungufu wa "vitu vya rohoni". Upungufu huu humsukuma mtu kuwa na njaa na kiu ya kumtafuta Mungu kwa moyo wote, nguvu zote, na akili zote. Kuna thawabu inayoambatana na Umaskini wa roho kama Biblia inavyosema ktk kitabu cha Mathayo 5:3;
... Heri walio maskini wa roho, kwa maana ufalme wa Mungu ni wao.
 
Ndugu mwandishi, leo umevurugwa haswaa
 
Kwanza usimsaidie mtu kwa mategemeo ya kukulipa fadhila msaidie mtu kwa ajili ya Mungu pili nikuulize ukiwa maskin then ukapata pesa hapo laana inakua imekwisha?
 
Huu uzi ungepewa title "NGUMU KUMEZA" coz unapapasa kwa undani mambo ambayo yana uhakika kwa 100%.

Mfano hai ni kwangu mimi....
Nina wajomba zangu watatu ambao ni matajiri sana dar es salaam.... Wako na uwezo mkubwa sana, wanamiliki ma sheli mengi, daladala za kumwaga, hoteli kama zote na mamiradi ya kufa mtu....
Kuna kipindi nikiwa nasoma, nlikuwa na uhitaji wa sh. Laki nane tu. Nikaona ninyanyue kwato zangu kuwatembelea ili kupata ka msaada. Majibu nlokutana nayo nkayapima kwa mizani, nikaona nabezwa laivu yani.
Mmoja alinambia kuwa hana laki nane ila nikiweza nikae kwenye moja ya nyumba zake kama mwangalizi then baada ya miaka mitatu ataninunulia pikipiki[emoji23][emoji23][emoji23]
Aki nliaga, na msaada nloulamba ni kupanda range rover hadi ubungo + kukatiwa tiketi ya kurudi nlipotoka[emoji23][emoji23]

Hii iliniumiza sana kisaikolojia bt nlikomaa nkaenda had chuo kikuu bt nliacha chuo nkajikita kwenye biashara.
Baada ya muda walipata habari zangu,. Wakanitafuta kunipa ABC za kupambana,.
Mafanikio yalivonitembelea wakawa ndugu zangu wa karibu sana, kiasi kwamba nikihtaji hata M kadhaa, kupata kwao sio taabu.

So kwa uzi huu, kuna mambo nmeelewa
 


Mimi mtu asiponisaidia ndio amenisaidia kujisaidia mwenyewe
 
Mtoa mada hajasema matajiri hawakosei (wao si malaika), wala hajasema lazima wawe na fedha nyingi, amezungumzia Kusengenya wengine, fitina,wivu, wizi, Fujo nk kama tabia za kimaskini

Tajiri wa pesa anaweza kuwa masikini pia
Ila masikini wengi zaidi wanatoka kwenye kundi la watu duni.
 
Nilikuwa najiuliza zangu hapa ety iv wote tukiwa matajiri dunia hii itakalika kwel? nakukumbusha tuu TANZANIA n miongon mwa nchi za ulimwengu wa tatu nchi maskin .
 
Tatizo sio ww tatizon kwa msaada wa watu wa marekan wanaokuletea msaada na ww unakubal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…