Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
USISHANGAE KUONA ALIYETAKIWA KUKUTETEA NDIO ANAHAMASISHA UPIGWE
Ukiona hayo usishangae hata kidogo kwa sababu yoyote anaweza kuwa yule usiyemtarajia kuwa.
Unaweza msaidia kiberiti awashe moto wa kupikia ila akimaliza tu mpaka kula anakuja na kiberiti kile kile kuchoma nyumba yako.
Atakupigia simu akiwa anaenda ili umuelekeze ila akifika tu kwanza hakwambii pili hapokei simu zako tena.
Leo unaweza mpa chumvi ila kesho akakuletea sumu kama shukrani.
Uliyempa ngazi atangulie kupanda juu akifika tu anatoa ili mwenye ngazi usipande.
SIKIA, HUU NDIO UHALISIA ULIVYO FANYA WEMA USIOWEZA KUKUFULISI
Tenda wema ila hakikisha unabaki na wema mwingine wa kukusaidia , ukimpa mtu ngazi apande juu hakikisha unabaki na ngazi nyingine ili akitoa nawe usipande basi utumie ile ya akiba.
Wema wako ukiisha wote usitegemee kusaidiwa na uliowapa na wakiwepo basi ni wachache sana hivyo usifanye DENI
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako