Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
USITAFUTE HESHIMA KWA WANADAMU!
Anaandika, Robert Heriel
Yule Shahidi,
Andiko hili ni Kwa watu wote!
Nimeona Vijana wengi wanapenda utukufu, wanapenda kuheshimiwa, wanapenda sifa. Hilo sio tatizo kwani ndio silika ya mwanadamu ilivyo. Lakini tatizo linakuja kuwa wanapenda mambo hayo kutoka Kwa Nani? Hapo ndipo lilipo tatizo.
Kupenda heshima kutoka Kwa watu ni kutafuta UTUMWA, kutafuta kujitesa, kutafuta wanafiki, kutafuta kuwapendeza wasio na maana yoyote.
Kamwe kwenye maisha usipende kuheshimiwa na kuzingatiwa na wanadamu. Hakuna lolote la maana utakalolipata,
Usisome ili uheshimiwe Bali soma ili upate Elimu na maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.
Usifanye kazi Fulani ili uheshimiwe, Bali fanya kazi hiyo Kwa ajili ya kuisaidia jamii na watu wako.
Usitafute pesa ili upate utukufu na kuabudiwa, Bali tafuta pesa ili utatue matatizo ya jamii inayokuzunguka.
Yeyote afanyaye Jambo ili apate heshima kutoka Kwa watu huishia kudharaulika, Kwa maana Kwa mwanadamu hakutoki heshima na binadamu sio kiumbe aliyeumbwa kumheshimu kiumbe mwingine.
Mwanadamu atakuheshimu akiwa na shida, ukimsaidia shida ikaondoka hatakuheshimu tena Kwa sababu binadamu hakuumbwa kutosheka hivyo hawezi kuwa na Shukrani yadaima.
Mwanangu, heshima ya kweli inatoka Kwa Aliyekuumba, ndiye Mungu mwenye Enzi, huyu akikuheshimu basi wewe ni kitu mbele ya USO wa Dunia hii. Lakini huyo akikudharau basi wewe sio lolote na kamwe hautakuwa lolote.
Ili Mungu akuheshimu lazima umheshimu,
Vile unavyopenda kuheshimiwa ndivyo na Mungu anavyopenda Umheshimu.
Kuna miungu mingi lakini miungu ya dhahiri ni pamoja na Baba na Mama yako, au walezi wako.
Hao Mungu Mkuu anakuagiza uwaheshimu, ili nao wakuheshimu. Naye Mungu akuheshimu.
Asiyeheshimu wazazi wake kwenye hii Dunia sio lolote hata kama anajidanganya na kujiongopea kuwa yeye ni lolote.
Usifanye maovu ukamuasi Mungu ili uheshimiwe na Watu, hawa wanaoenda chooni kunya mavi ndio unatafuta heshima kwao, hawa wanaolala usiku hawajitambui ndio unahangaika kuwafurahisha, hawa ambao ni vigeugeu Kama kinyonga ndio unataka wakuheshimu, kuwa Sirius mwanangu.
Fanya kazi Kwa bidii, ridhika na ukipatacho. Usipende kuzingatiwa na kujifananisha, maisha hayahitaji kutumia nguvu nyingi, hayahitaji kulazimisha,
Sijui huna nyumba, sijui huna Gari, sijui siku zinaenda, sio kazi yako kuhesabu siku na kujua mambo ya kesho.
Fanya wajibu wako, tenda Kwa akili.
Usikubali maoni ya watu yakuendeshe,
Naona Vijana wengi wanaingia kwenye Sonona"depression" na kukata tamaa ya Maisha, maisha ni zaidi ya nyumba, pesa, au Mke au Mume.
Ikiwa njia ya maisha yako imekuwa hivyo ilivyo usijali, usikate tamaa, wala usijiingize kwenye mkumbo wa kutaka kushindana na walimwengu ili kutafuta heshima ya Dunia ambayo ni ya uongo(mpito) siku zote uongo haudumu, ukweli unadumu, usipende wala usiendekeze Jambo ambalo halidumu.
Furahia Yale yote uliyonayo, kisha yatafute usiyonayo Kwa kutumia uliyonayo Kwa kulinda heshima ya Mungu ili naye akuheshimu.
Ukitafuta kuheshimiwa na Watu utajiingiza katika Mkondo WA kujidhalilisha, kujitoa utu wako, kutoa utu WA wengine Kwa kuwadhuru na kuwadhulumu,
Unadhulumu wengine Kwa Siri ili upewe heshima na watu wengine hadharani, huko ni kujidanganya na Dalili ya mtu aliyechanganyikiwa na Mpumbavu.
Unauza madawa ya kulevya Kwa Siri ili upate pesa ukidhani unapewa heshima hadharani lakini siku zote heshima ya mtu IPO katika dhamiri yake mwenyewe.
Ni Sawa na Mtu aliyeibia mtihani alafu akafaulu unafikiri atajiona anaakili Kwa vile watu wanamuona hivyo, Hasha! Dhamiri yake ya ndani itamuambia yeye ni mjinga tena mjinga wa mwisho.
Kiongozi heshima yake IPO katika kuongoza Kwa Haki, bila kudhulumu. Lakini viongozi Kwa kutaka heshima isiyokuwepo wanaiba na kudhulumu watu wa nchi Yao waliopewa wawatumikie, wakidhani kuna lolote watakalolipata,
Jambo lolote lililotengenezwa na Mwanadamu halimfanyi mwanadamu kuwa na heshima, iwe ni Pesa, magari, nyumba, simu na mambo yote yaliyotengenezwa na binadamu hayamfanyi mtu kuwa na heshima au thamani.
Watawala wote wenye akili za juu na hekima tangu zamani walilijua Jambo Hilo kuwa Vitu vya kutengenezwa na binadamu sio vinavyompa Kiongozi heshima isipokuwa, Tabia na Falsafa njema ya Kiongozi ndio humpa heshima Mfalme au Mtawala.
Vitu vya binadamu alivyounda vinapita kadiri ya Zama na kizazi lakini Falsafa na Utu wema kamwe haupiti.
Kufurahia maisha sio kuhangaika na Dunia, kufurahia maisha ni kuishi Kwa Upendo na watu wote na kuhakikisha Amani ya kweli inatawala. Na Amani ya kweli ni Ile ya kuhakikisha kila mtu anapewa Haki yake, na kila mtu anabaki katika mipaka yake.
Mkubwa abaki kwenye ukubwa, na mdogo abaki kwenye udogo wake.
Mwanaume abaki kwenye Uanaume wake na Mwanamke abaki kwenye uanamke wake.
Swamwel aliandika; Mungu atamheshimu atakayemheshimu, na atamdharau atakaye mdharau.
1 Samweli 2:30
Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.

Ni bora utafute kuheshimiwa na MUNGU aliyekuumba kuliko kucheza michezo ya kitoto Kama Mpumbavu asiye na Akili.
Nipumzike sasa,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam