MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Takwimu zinaonyesha kwamba aslimia 75% ya fedha zinatolewa kwa Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) hutoka kwa mtu mmoja mmoja (Individual Donors) na asilimia zinazobaki hutoka kwenye Taasisi. Ukweli huu usikufanye uamini kwamba kila mtu utakaemuendea kwa ajili ya ufadhili ataifadhili Taasisi yako, LAA HASHA.
Ili mtu aweze kufadhili Mradi au Programu inayoendeshwa na Taasisi yako, ni lazima vigezo vitatu vitimie, ambavyo ni;
- Kuwe na maslahi juu ya kile kinachofanywa na Taasisi
- Mfadhili awe na uwezo wa kuchangia
- Kuwe na kiunganishi kati ya Mfadhili na Taasisi
Kumjua Mfadhili sahihi wa Taasisi yako, hatua ya kwanza ni kuzingatia vigezo nivyoandika hapo juu, pili kuandaa wasifu wa mfadhili yaani "Donor Profile" Uandaaji wa "Donor Profile" hautofautiani sana na utafiti wa soko juu ya huduma au bidhaa fulani (market research) Kama ilivyo katika biashara, Taasisi inapaswa ijue exactly wapi na kwa nani inapaswa kuuza mradi au programu yake. Kujua taarifa muhimu za mfadhili wako ni muhimu sana. Katika uandaaji wa "Donor Profile" ni muhimu kujumuisha taarifa zifuatazo
- Kipato cha mfadhili
- Kiwango cha Elimu ya mfadhili
- Kazi au Taaluma ya mfadhili
- Hali ya kifamilia ya mfadhili (ameoa, hajaoa)
- Uzoefu wa mfadhili juu ya yale yanayofanywa na Taasisi
- n.k
OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA