Usitumie hela nyingi kwenye mwonekano wa duka badala ya bidhaa.. weka stock ya kutosha.

Usitumie hela nyingi kwenye mwonekano wa duka badala ya bidhaa.. weka stock ya kutosha.

Tatamobitch

New Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
4
Reaction score
11
Kwa Tanzania hasa kwenye miji mikubwa hili limekuwa tatizo kubwa. Wafanyabiashara wadogo tena wanaoanza biashara utakuta wanatumia hela nyingi za mtaji kuwekeza kwenye mwonekano wa duka badala ya bidhaa anazouza.

Vijana wengi hasa kwenye biashara ya nguo wamejikuta wanafunga biashara zao chini ya miezi sita toka waanze kwa kosa hilo la kiufundi. Hakuna ubaya wowote katika hilo ila inaweza msababishia hata presha mhusika kwasababu hela kaitumia kwenye kitu alichoona sahihi ila mambo yakaenda tofauti.

Mimi nashauri vijana wote wadogo wanaoanza biashara wasikimbilie kufungua maduka... waweke nguvu online zaidi kwasababu gharama za kuwa na duka kwa Tanzania ni kubwa sana kwa nyakati hizi.

Hizo hela za kufungulia duka nunua vitu vinavyopendwa na wateja wako kisha wauzie online. Mtaji ukiongezeka basi wafungue duka. Ila kama ikiwezekana vijana wanaweza wakaungana wakashea frem moja.

Ikiwa ni peke yake basi kijana asikimbilie kufanya sana decorations ya frem na badala yake aweke mzigo wa kutosha ili aaminike kwa wanunuzi. Mteja akija hanunui decorations zako. Mwonekano wa duka unaufanyia kazi taratibu huku biashara ikiendelea.

Pia ikumbukwe baadhi ya wateja wakiona duka zuri sana huogopa na kuhisi bei za vitu itakuwa kubwa.

Pia nashauri wale wanaofungua maduka waonekane kwa wenzao kwamba ni wapambanaji waache huo upuuzi mara moja. Kuna katabia ka kutumia pesa nyingi kwa kile kinachoitwa ufunguzi wa duka.

Shampeni hununuliwa kabisa huku marafiki toka sehemu mbalimbali wakiwa wamealikwa. Haihitaji utafiti wa kisomi kujua ni wangapi wenye tabia hii walifeli mapema. Wadogo zangu ishini kwenye uhalisia wenu usiige.

Vunjabei anavyofanya sherehe za uzinduzi ni kwamba safari ilianzia mbali sana.
 
Kwa namna fulani nimekuelewa, ila kuna baadhi ya biashara za online mteja atataka aje ofisini, mfano mtu unauza Laptop Used, umepata mteja anataka aje ofisini utampeleka wapi. ? Ukimwambia ivo ataona kama utapeli flan..

Mimi naona uzi wako uko selective sana, labda kwa baadhi ya biashara itafaa
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Ninayo app nzuri ya kupiga mahesabu ya duka.Inafaa kutumia wakati wa kufanya stock.
1.Unaweza kujua duka lako limekuingizia sh. kwa mwezi au kwa mwaka.
2. Inaonyesha thamani stock iliyopo dukani
3. Inaonyesha Kila bidhaa unayouza Ina faida ya sh. ngapi
4. Kama Kuna upotevu wa fedha inaonyesha.

INAFAA KUTUMIA KWENYE SMART PHONE AU COMPUTER

Ili kuitumia unatakiwa kuwa na rekodi sahihi za Kila manunuzi na mauzo ya Kila siku. Nicheki Whatsapp 0753546162
 
Uzi mzuri. Huu upuuzi unafanywa na vijana wengi sana. Wanatia hela nyingi mno kwenye kupamba duka matokeo yake ndani ya miezi 3 kilio.
 
Kupamba biashara/duka ni njia ya kukaribisha TRA wakupige ya kichwa...
 
Back
Top Bottom