Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Naandika katika hali ya masikitiko makubwa kutokana na uzoefu wa madhila ya kimaisha niliyoyapitia na ninayowaona wengi tukipita katika njia ileile ya majuto kwa lengo kuu la kuhakikisha hatuupotezi muda mfupi tuliojaliwa na Mungu kufanya mambo yasiyo na faida yoyote kwetu.
Ni sahihi sana kuwa mtu wa watu, kuwapenda watu, kuwatendea vizuri lakini siyo sahihi hata kidogo kuwa vile wanavyotaka wao uwe Ili wao wafurahi. Kosa kubwa ninaloliona ni hali inayoweka thamani kutoa na kukiacha kinachotoa kana kwamba hakina kusudi la uwepo wake au hakina upekee wake.
Wapo waliojibadili sura, waliojitahidi kuwa katika muonekano fulani ambao kwa hakika siyo wao ila ni kwa lengo la kuwafurahisha watu fulani au kumfurahisha mtu. Hapa kuna maumivu makali ya ndani kwa sababu ya ushindani kati ya kinachotendeka na uhalisia wa ndani. Wengi wetu tunavyojionesha kwa watu sivyo tulivyo ila ni vile tunavyoamini itawafurajisha ila kiuhalisia sisi hatufurahi.
Jamii imetunyang'anya kilicho chetu na kutufundisha kufanya inachotaka ikione. Siyo jambo la ajabu mtu kuishi katika Dunia ya leo kwa muda wote atakaojaliwa na kutokuishi maisha yake kabisa mpaka akafa. Wachache wanaoitambua siri hii huonekana wakosaji, watu wanaojipenda kuliko wengine na sifa nyingine mbaya.
"Ukitaka kuwa kama tai usifanye nazoezi na bata"