Usiwe mwepesi wa kuhukumu….. kwa sababu huwezi jua wenzako ni kwa nini wako na hali unazoziona

Usiwe mwepesi wa kuhukumu….. kwa sababu huwezi jua wenzako ni kwa nini wako na hali unazoziona

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Daktari mmoja aitwaye Abuu aliingia hospital kwa
haraka baada ya kupigiwa simu kuwa alitakiwa
kwa
ajili ya operesheni ya haraka sana.Moja kwa moja
bila kupoteza muda Dr Abuu aliingia katika
chumba
cha
upasuaji.Akamwona baba wa kijana aliyetakiwa
kufanyiwa upasuaji akiwa katika chumba cha
kusubiria. Baada ya kumwona Dr Abuu baba wa
kijana alipiga kelele huku akimfuata na
kumwambia:
“Kwa nini umechukua muda mrefu kuja? Haujui
kuwa mtoto
wangu angeweza kufa? Una chembe ya
ubinadamu wewe au kwako vifo ni ufahari?”
Abuu alitabasamu na kumwambia Yule baba:
“Sikuwa hapa hospital ila baada ya kupigiwa simu
nimekuja haraka kama nilivyoweza…… Nakuomba
samahani na uwe mpole nifanye kazi mara moja”
“Niwe mpole?! Ungekuwa wewe ndio mimi na
mototo wako anataka kufa na daktari anakuambia
uwe mpole ungekuwa mpole? Aliongea baba Yule
akiwa na hasira za kutisha.
Daktari Abuu alitabasamu tena na kumjibu mzee
yule: “Nitasema maneno yaliyopo kwenye kitabu
kitakatifu “Tuliumbwa kwa mavumbi na tutarudi
mavumbini, Jina la bwana libarikiwe”. Daktari
hawezi
kurudisha Maisha ya mtu bali kwa neema zake
bwana. Mwanao atapona kwa jina la bwana.
“Huwezi kunipa ushauri wakati wewe sio
mwajibikaji
hivyo huna maana” Aliongea baba kwa hasira
Upasuaji ulichukua masaa kadhaa na baadae
daktari
Abuu akafungua mlango na kutoka akiwa na uso
wenye furaha na kumwambia baba “Ashukuriwe
Mungu mtoto wako kapona na bila kupoteza
muda
Abuu akaondoka kabla ya Yule mzee hajadadisi
zaidi.
Mbona huyu daktari mkorofi sana, yaani hata
kabla
sijamaliza kuuliza kaondoka? Aliuliza yule mzee
kwa
nesi aliyekuwa pembeni yake.
Nesi akamjibu huku machozi yakimtoka: “ Mtoto
wa
daktari huyu alipata ajali na kufa jana, Alikuwa
nyumbani akijiandaa kwenda kumzika,Na kwa
kuwa hakuna daktari wa tatizo hilo zaidi yake basi
tukampigia ndio akaja mara moja na sasa
anawahi
kwenda kumzika mwanae.”
Funzo :
Usiwe mwepesi wa kuhukumu….. kwa sababu
huwezi jua wenzako ni kwa nini wako na hali
unazoziona zikiwaandama au watu wanapitia
Maisha
ya namna gani wakijitahidi kukufanya wewe uwe
na
furaha na amani.
 
Those ideal people.. Easy to hear about them but almost impossible to find one..!
 
watu wenye haraka na kupanic bila hekima inatugusa.tunataka vitu kama hvi humu jf,siyo porojo.
 
Hili ni fundisho tosha kwetu sie wanadamu! wengi wetu ni wepesi mno wa kulaumu bila kutaka kujua kisababishi!niliwahi kusoma story hii somewhere ila sikumbuki km ni jf au kwingineko maana twapitia mitandao mingi ya kijamii! ila kwa umuhimu wa funzo lililomo ndani ya story hii,hata iandikwe mara elfu ni sawa tu !
 
Ni kweli kabisa hii story hata mi imenigusa mi nimekuwa ni mwepesi sana wa kuhukumu thanx mkuu kwa story nzuri ntajifunzia kutokea hapo
 
::::nodding my head:::::

Muiteni mpigamsuli ,itamsaidia sana....
 
Last edited by a moderator:
huyo mzee hayupo sawa upstairs,.naye angepata tiba pia,.

Kama huyu mzee hakuwa sawa upstairs basi asilimia kubwa ya watanzania hawako sawa upstairs!Yaani hana tofauti kabisa na watanzania walio wengi.Tofauti tu ni huyu daktari,wengi wa madaktari wetu ukionesha kutokuridhika tu,achilia mbali kulaumu wazi wazi,anaweza kuzira ama kukujibu vibaya ambavyo hutasahau

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom