Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Anaandika Alexandr Solzhenitsyn kwenye Gulag Archipelago.
Anasema kuwa wakati wa ukomunist huko USSR kulikuwa na mambo ya kushangaza sana.
Siku moja katibu wa chama alitembelea mji fulani. Ndani walijaa watu mashuhuri wa ule mji na kama kawaida, KGB nao walikuwa ndani. Kabla ya kikao kuanza wakaanza kupiga makofi kumsifu kiongozi wa nchi kwa mafanikio waliyofikia.
Wakasimama na kuanza kupiga makofi. Wakapiga makofi na kupiga. Kadri muda unavyoenda ndipo yule katibu akawa anakazana kupiga makofi. Kila mtu alikuwa anaogopa kuacha kupiga makofi, hivyo walipiga kama dk nzima au mbili hivi. Sasa mwalimu mkuu wa shule moja akaona huu ni upuuzi. Akaacha kupiga makofi na kukaa. Hapo na wengine wakafuata.
Kesho yake KGB wakamfuata na kumuexile huko Siberia na kumwambia. " Siku nyingine usiwe wa kwanza kuacha kusifia"