Usiyoyafahamu kuhusu maandalizi ya AFCON

Billal Saadat

Senior Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
169
Reaction score
358
AFCON BID 2027 (IPO NAMNA HII).

Tanzania, Kenya na Uganda zimeungana kwa lengo la pamoja la kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika 2027. Afrika haijawai kuwa na maandalizi ya pamoja huko nyuma michuano ya Afrika.

VIGEZO VYA KUANDAA AFCON
Ili nchi iwe mwenyeji wanahitaji kuwa na viwanja sita vilivyopewa hadhi na CAF kwa Tanzania tunavyo vinne(Mkapa, Karume, Azam pamoja na kirumba) hivyo kwa uandaji wa pamoja kwa Afrika mashariki Kenya na Uganda watajumuisha vya kwao kama kuna maboresho yatafanyika.

Viwanja vyetu tulivyonavyo vitahitaji maboresho pamoja na kama hilo linawezekana tunaweza kupata uwanja mpya why not.

NINI MAANA YAKE?
Nchi za Afrika mashariki kwa mara ya kwanza na Afrika kwa ujumla zimeungana kuandaa michuano ya mataifa ya Afrika kwa Mwaka 2027 kuungana huku kunafanya kupunguze competition ambayo ingeweza kutokea endapo Kenya na Uganda zingetaka kushiriki peke yake kwa kuungana kumefanya iwe strong bid interms of kura zitakazopigwa na nchi mwanachama.

CAF WANACHAGUA VIPI MSHINDI
Moja watakagua viwanja kama idadi ya viwanja vimetimia kwenye hili linatoa sasa maboresho kwa nchi kuaanda viwanja vingine zaidi endapo watapa nafasi ya kuwa waandaaji.

Hali ya usalama na miundombinu ya nchi waandaaji wa michuano husika

Hamasa ya kimichezo kwa nchi husika hii ni point kubwa sana.

Bid ya AFCON ni kama uchaguzi tu mwenye ushawishi na aliyefanikiwa kuwashawishi wale wapiga kura katika Bid ndiye anayepewa nafasi ya kuandaa mashindano.

FAIDA ZA KUANDAA AFCON ZAIDI YA NCHI MBILI
Ushirika wa kuomba kuanda michuano mikubwa kama AFCON kunatoa nafasi ya nchi kujianda kwa uzuri sababu mnagawana shughuli za kufanya katika maandalizi. Less infrastructure to build/renovate for each nation

Bid ya pamoja inatoa nafasi kwa nchi mwanachama wa CAF kupata nafasi ya kuchaguliwa na wanachama washirika wa pamoja.

Kuongeza mauzo ya tiketi kwa timu zilizopo nyumbani nchi muandaaji.

Kupunguza overall risk of hosting for each nation itapunguza mizunguko kila nchi kuwa inaanda peke yake.

THAMANI ITAKAYOPATIKANA
Kwanza inajenga international profile ya nchi.

Inavutia wawekezaji wengi wa sekta za michezo makampuni kama Puma, Nike na Adidas.

Inasaidia kukuza vizazi vya soka itavutia scout wengi kuja kutazama na kusaka vipaji afrika mashariki.

KIUCHUMI
Ongezeko la Viwanja vya michezo

Ajira kulingana na mahitaji ya michuano za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Inakuza Utalii wa ndani na nje ya nchi

Inakuza mahusiano ya kimataifa

Inaongeza mzunguko wa fedha na kukuza mnyororo wa thamani wa bidhaa na uchumi.

Inakuza lifestyle na utamaduni wa nchi husika

NB AFCON ni mashindano makubwa sana na fahari yetu kuona Tanzania inapata nafasi ya kuwa muandaaji wa mashindano husika. Suala lililopo ni kuboresha viwanja tu na miundombinu kwa nchi zilizokwisha omba nafasi.

Mungu ibariki Tanzania, Mama Yuko Kazini.
 
Why not us? Hiii campaign ngoja tuone itafika wapi?
 
Hv kenya si kafungiwa na fifa kisoka.
 
Ndio gharama ya Bil 600 mkuu?
Are we serious by anymeans?

Hiyo hela ni sawa na km 600 za lami.

Na inatosha kuipa kila wilaya km 2 za lami.

Possibly ni Campaign za 2025
 
Nyongeza tu
1. Kiwanja cha Amaan Zanzibar kipo kwenye bid. Toa Kirumba na Azam. Promise ni kujenga kipya Arusha.

2. Botswana na Algeria ndio wenye bid za kushindana na Pamoja bid ya EA.

3. West and North Africa hosted a lot. Our slogan BRING AFCON TO EAST may dilute Algeria bid. But Kenya was given hosting opportunities more than once and bowed out, so may dent pamoja bid.

4. Botswana is less populous and less football intensity.
 
Sasa hivi tunaangalia fainali za jumapili za Yanga

Kama nchi imeandaa nini kuonyesha dunia? Kama Yanga wamejiandaaje kuonyesha uzalendo wa kitanzania?
Tulianda hapa finals za u17 ilikuwa kichekesho yaani nchi unaingia toka airport mpaka pale kilimanjaro hm a dalili za kuonyesha hawa ni wenyeji wa michuano
 
Tulianda hapa finals za u17 ilikuwa kichekesho yaani nchi unaingia toka airport mpaka pale kilimanjaro hm a dalili za kuonyesha hawa ni wenyeji wa michuano
Fainali kama hizi, huwa ni tukio la KITAIFA, ndio siku ambayo nchi inaonyesha dunia utajiri wa utamaduni wake na sio kuchukua hivi visanii vibana pua hakuna. Unaandaa kitu unique ambacho ni tofauti na wafanyavyo nchi nyingine
 
Wasiamamizi wa vuwanja wakiwa na mfumo ule wa umeme kukatika hovyo inaweza kutia doa endapo CAF watakuwa curious zaidi
 
Tulianda hapa finals za u17 ilikuwa kichekesho yaani nchi unaingia toka airport mpaka pale kilimanjaro hm a dalili za kuonyesha hawa ni wenyeji wa michuano

Hata huko Ulaya Tournament za under age hazina viwango hivyo compare na mashindano makubwa sababu popularity yake bado ipo chini.
 
Wasiamamizi wa vuwanja wakiwa na mfumo ule wa umeme kukatika hovyo inaweza kutia doa endapo CAF watakuwa curious zaidi

Mashindano ni 2027 kuna maandalizi makubwa hapo kati yatafanyika na maboresho.
 

Well.
 
Mashindano ni 2027 kuna maandalizi makubwa hapo kati yatafanyika na maboresho.
Hakuna cha maboresho yeyote sijui ni nani amemshauri mama akubali


Kiwanja chenye international FIFA standards kipo approved Ni kimoja nacho kina kasoro chungu nzima kikiwa ni taa na umeme kiufupi matukio ya mechi ya yanga na river United pamoja na Uganda vs Tz yametutia aibu kama taifa


Hivyo wiwanja vya ccm kirumba au Azam na karume sio hadhi ya mechi za kitaifa

Hakuna viwanja vya mazoezi maana afcon sio vya kuchezea tu hata vya mazoezi vinatakiwa viwepo wydad wamekuja kocha wao alilalamika sana ilikuwa ni aibu


Hatuna miundombinu hiyo na naomba Mungu north Africa washinde bid tuondokane na aibu hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…