Usiyoyajua kuhusu Nyuzinyuzi katika Vyakula

Usiyoyajua kuhusu Nyuzinyuzi katika Vyakula

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Vyakula vya watu wengi wanaoishi katika miji hapa Tanzania ni vile vinavyotokana na wanyama kama nyama, maziwa, samaki, kuku, mayai, dagaa, soseji na vyakula vilivyotengenezwa kwa kutumia nafaka zilizokobolewa. Vyakula hivi havina nyuzinyuzi za kutosha.

Nyuzinyuzi kwa kitaalamu dietary fibers zinapatikana kwa asili katika vyakula tunavyokula vinavyotokana na mimea.

Hii ni sehemu ya vyakula vya mimea ambayo tumbo la mwanadamu haliwezi kusaga, kwa hiyo inatoka kwa kupitia haja kubwa kama kinyesi.

Kuna aina mbili za nyuzinyuzi, inayoyeyuka na isiyoyeyuka katika maji.

Aina zote mbili ni muhimu kwa afya ya binadamu kwa kusaidia usagaji wa chakula, kuzuwia magonjwa ya moyo, kisukari, uzito kupita kiasi, saratani ya utumbo mpana na kukosa choo kikubwa.

Nyuzinyuzi zinaondoa sumu na uchafu kutoka tumboni, zinasafisha tumbo na ni chakula cha bakteria wazuri wanaoishi tumboni.

Nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinanyonya maji na kutengeneza kitu laini tumboni ambacho kinapunguza kasi ya usagaji chakula tumboni. Ndiyo kusema,
nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinamfanya tumbo kubaki na chakula kwa muda mrefu.

Mlaji anaepuka kula mara kwa mara na hata kuwa na uzito kupita kiasi.

Kupunguza kasi ya kusaga chakula tumboni pia, kuna saidia kupunguza wingi wa sukari katika damu. Kwa hiyo dawa ya insulini inayozalishwa mwilini ili kupunguza wingi wa sukari katika damu, itaendelea kufanya kazi vizuri na kumwepusha mtu na ugonjwa wa kisukari.

Vilevile, nyuzinyuzi zinazoyeyuka zinaufanya utumbo kunyonya kiasi kidogo cha mafuta aina ya lehemu yanayotokana na vyakula. Matokeo yake mwili utakuwa na kiwango kidogo cha aina mbaya ya lehemu, inayochocheavmagonjwa ya moyo.

Nyuzinyuzi zinazoyeyuka katika maji zinapatikana kwa wingi katika maharage, karoti, matango na matunda yakiwemo machungwa, epo, peasi na strawberries.

Kazi kubwa ya nyuzinyuzi hizi ni kuongeza ukubwa wa mabaki ya chakula kisichosagwa na kutoka nje kama choo kikubwa kwa wepesi. Kwa hiyo, zinaondoa tatizo la mtu kukosa choo kikubwa na kuufanya utumbo kufanya kazi vizuri.

Chanzo kizuri cha nyuzinyuzi zisizoyeyuka ni nafaka zisizokobolewa na mbogamboga.
Mahindi na ngano zisizokobolewa,karanga, mbegu, mchicha, kabichi,vitunguu, nyanya na matunda ya aina mbalimbali.
Wasomaji wazingatie kuwa aina zote mbili ya nyuzinyuzi ni muhimu kwa afya.

Watu wale aina mbalimbali za matunda, ml mbogamboga na nafakavzisizokobolewa ili kuzipata aina zote mbili. Kuna watu wanatumia nyuzinyuzi zilizo tengenezwa kutokana na mimea. Watumiaji wa aina hiyo ya nyuzinyuzi, wawe wanakunywa maji mengi kwa kila siku na waombe ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya mara kwa mara.

Source: Mwananchi NP
 
Mkuu picha ya nini wakati kika kitu kinajieleza hapo!!
But kwa faida yako na wengine angalia matunda haya, unapokula ndizi kuna nyuzi ambazo ubaki kwny ganda ila chungwa huwa unakula hizo nyuzi direct pasi kujua.


akyanani mkuu weka picha walau unishawishi hapa please ka picha
 

Attachments

  • 1427460373653.jpg
    1427460373653.jpg
    26.3 KB · Views: 277
  • 1427460396101.jpg
    1427460396101.jpg
    14.1 KB · Views: 93
Back
Top Bottom