Mhandisi Mzalendo
JF-Expert Member
- Aug 23, 2010
- 6,682
- 11,461
Habari,
Nchi nyingi zina utaratibu, mila na desturi za maisha. Kutokana na kuzunguka sehemu mbali mbali leo nmeonelea nikuambie yale yahusuyo Senegal (LAND OF TERANGA kama wanavyojiita yani ardhi ya UKARIMU) ambayo ni tofauti kidogo na nchi yetu ya Tanzania.....
VISA ya Senegal kwa Mtanzania ni on arrival. Ukishaingia Senegal hamna anayekufuatilia ilimradi uwe na passport yako. Visa ikiexpire haubugudhiwi na yeyote. Labda uchokoze mamlaka....
Ila ni vyema kugonga VISA ikiisha.
1. DINI
Upande wa dini waislamu ni asilimia 90 na wakristo ni asilimia 10.
Hii kwa kiasi kikubwa ni nchi iliyojaaliwa kuwa na waislam wengi pamoja na kuwa ilitawaliwa na wafaransa.
Tamaduni za waislam hapa ni tofauti sana na kwetu.
●Wana mji wao mtakatifu unaitwa Touba. Kila mwaka hukutana kwa ajili ya Maulid pale Touba. Maulid hiyo utambulika kama GRAND MAGAL OF TOUBA wanakutana takribani watu milioni 2-3, huduma za kijamii zote huwa bure kuanzia kulala, kula n.k ni siku muhimu sana kwa waislamu wa Senegal Huko asilimia kubwa ya huduma ni bure na ni mji unaojitawala. Maulid hii hubadilika tarehe kila mwaka kutokana na kalenda wanayotumia ni Islamic calender ambayo ina tofauti na Gregorian Kalenda kwa takribani siku 11....
Touba wanapatikana masheikh wakubwa na watu wanaoitwa Marabuuu... Wanamiliki madrasa ambazo watoto kuanzia wadogo wanalelewa huko.
●Uislam ni mtindo wa maisha kwao ni utamaduni wao. Wanauishi uislamu na uislamu unaishi ndani yao kwao ni zaidi ya imani... Ni utamaduni wao.
●Wanaswali sehemu yoyote muda wa kuswali utakapomkutia. Si barabarani, beach, kituo cha daladala au sehemu yoyote. Usishangae kukuta sehemu wanawake wanajiuza halafu kuna mtu katandika mswala wake anaswali bila bugudha.
●Wanawake waislamu hawavai hijab, nkabu wala chochote wao vazi lolote twende. Ikifika muda wa swala atatoa mtandio wake na kanga atajisitiri anaswali.... Same kwa wanaume. Senegal mpaka wahuni wanaswali.
●Asilimia kubwa hamna ubaguzi wa dini.
2. AMANI
Ni nchi yenye amani kwa kiasi kikubwa na utulivu siasa zao za kistaarabu ingawa kwa sasa Rais aliyepo anamtia kashkashi mpinzani wake Osuman Sonko kashapewa kesi za kutosha.... Siku wakiandamana wapinzani ujue shughuli zinafungwa town.
3. UHALIFU
Kuna asilimia ndogo sana ya uhalifu unaweza kusahau simu yako maeneo kama kariakoo au club au gym na ukaikuta pale pale. Sisemi hakuna wizi ila ni asilimia chache sana.
Magari mabovu yamezagaa mitaani lakini hutaona mtu kachomoa side mirror wala chochote...
4. MAKAZI
Mji mkuu Dakar ni mji wa gharama kubwa sana. Bei ya ardhi haikamatiki. Mji umejaa wote na nyumba zinazojengwa ni maghorofa tu. Ukiwa na kiwanja unajenga chote mpaka kwenye mpaka na mwingine anakuja kuunga nyumba yake. Asilimia 95 ya nyumba hazina fense wala parking. Kiwanja kinajaa nyumba.
Kukodi nyumba ni gharama sana kwa Senegal ukifananisha na TZ.
Nyumba nyingi kwenye makazi ya watu wa hali ya kati na uswahilini hawapigi plasta. Ukiangalia ujenzi wao utadhani ni majengo dhaifu ila wao system ya ujenzi wao ni tofauti na bongo.
Dakar imeathiriwa sana na chumvi. Hawatumii bati zinaoza.
Kwa sasa kuna ujenzi unaendelea wa satelite city eneo la djamniado ili ku offload Dakar city centre... Tuseme kama Dar na kibaha hv... Mji mpya unajengwa......
5. VYOMBO VYA USALAMA NA ULINZI
Askari wapo kwa ajili ya kulinda amani na raia. Hawana shida na yeyote. Ukikosea wanakurekebisha. Usipowagusa hawana habari na yeyote. Unaweza kukaa miezi hata kusimamishwa na traffic usisimamishwe. Unaweza safiri Dar to Mbeya hakuna wa kukusimamisha.
Usishangae kukuta mwanajeshi na raia wote wamevaa gwanda wanapiga story.
Au konda kavaa gwanda za jeshi (si za nchi yao) na hakuna shida.
6. MIUNDOMBINU
Barabara za mjini zimejengeka vilivyo. Kuanzia flyover, bypass n.k ujenzi unafanyika kila sehemu.
Wana barabara za kulipiwa ambazo zinamilikiwa na serikali, kampuni binafsi na wafaransa.....
Alternative way zipo ila foleni sana. Ukifika chagua kupita barabara za kulipia...
Umeme na maji ni nadra kukatika.
Pia Dakar ina udhaifu mkubwa kwenye miundombinu ya mifereji. Ukija kipindi cha mvua utapachukia. Maji yanajaa sana barabarani na kwenye makazi ya watu. Nadhani pia kwa kuwa wapo karibu na bahari....
7. MICHEZO
Wananchi wa Senegal wanapenda kufanya mazoezi sana. Usishangae beach zao kujaa watu wanafanya mazoezi. Barabara zimejaa watu wanafanya mazoezi. Wao ni mazoezi na mazoezi na wao.
Tofauti yao ni kwamba hawaendi viwanjani kuangalia michezo. Pamoja na kuwa na viwanja vingi. Wachezaji wengi wanatoka kwny academies... Hata ligi zao si maarufu kwa wasenegal wengi.
Ndio maana timu ya taifa inafanya vyema kuliko klabu....
8. VYAKULA
Bora umnyime chochote msenegal kuliko mkate. Ukienda mgahawani cha kwanza ni mkate kabla ya kula. Mkate ni deal.
Wana vyakula vingi maarufu kama Chepujam n.k.
Hakuna ugali na wanaushangaa
Kitunguu kwao kipo kwenye kila mlo.
Wanapenda kahawa sana na sukari.
9. STAREHE NA POMBE
Hivi vinapatikana sehemu zinazokaliwa na watu wa nje. Sehemu kama almadies, mji wa St. LUOIS. Sehemu kubwa ya Senegal hawauzi pombe. Klabu zao zinafunguliwa saa 6-9 Jumatatu asubuhi saa 1 unakutana na makundi ya vijana wanatoka klabu.
sigara zake makasha yana picha za kutisha sana .
10. LUGHA
Waliosoma wanajua kifaransa, wananchi wengi wanaongea WOLOF ingawa si wote.
Lugha ya ofisini ni kifaransa...
11. UWEPO WA WATU KUTOKA EAST AFRICA
Jamii ya watu kutoka East Afrika ni wachache sana. Unaweza kukaa miezi 6 ukakutana na mmoja. Watanzania almost hakuna bora Wakenya.
Msanii maarufu wa East Afrika ni Diamond Platnum. Na watu wanamjua Shilole na nyimbo yake ya Chura kuliko hata Ali Kiba.
Wanamkubali sana Magufuli.
Zanzibar ni maarufu sana.
Sheikh Sharif anajulikana sana na ni maarufu mno.
Simba inajulikana kuliko Yanga kwanza Yanga hawaijui kabsa... Big up kwa Simba wanawakilisha.
12. UVAAJI WA HIRIZI, SHANGA VIUNONI WAZIWAZI NI KAWAIDA
Usishangae kukutana na mtu kajitwisha hirizi yake na hana muda na mtu. Hii inanikumbusha yule mchezaji wa Simba Pape N'daw kutoka Senegal alikutwa na hirizi kwenye moja ya mechi. Kwao ni kawaida kama bangili.
Au mwanamke kavaa shanga zake kiunoni na top na wala hamna muda na watu hawashangai.
Pia ni nadra kuona mwanaume anapishana na mwanamke na kumuangalia.
13. KAZI MWISHO IJUMAA
Ni nadra sana kukuta ofisi imefunguliwa jumamosi yani hata kwa ofisi za madalali weekend wanafunga tofauti na kwetu kwenye real state agencies wao weekend ndio biashara inanoga.
14. SHULE
Wanafunzi wa shule nyingi hawavai uniform ni mara chache sana. Shule hufungwa kipindi cha mvua. Yaani kuanzia july mpaka September.
Sijawahi ona watu wanaogopa maji kama wasenegal. Dereva akiona kadimbwi anageuza na hawapiti hapo. Sijui nini kiliwahi wakumba.
N.k n.k n.k
15. USAFIRI WA UMMA NA BINAFSI
Usafiri wa umma kwa Senegal yaani daladala na Tax ni magari yaliyochoka. Unaweza kushuka airport pale ukakuta Tax zimechoka hatari usifikiri utatafuta na kupata mpya hizo ndio zilizopo, atleast siku hizi uber yao (YANGO) wanaingiza gari mpya.
Daladala ndio usiseme.
Wanatumia pia farasi kama usafiri anafungwa tela.
Magari binafsi huwezi kuingiza gari kuu kuu mwisho miaka mitano.
Brand za magari ni EUROPEAN. Toyota ni za kutafuta na pia ni ghali kwa kuwa zinatoka Japan Mbali.
Magari yao ni LHD
16. AJALI
Senegal hata ukinunua gari leo kesho unaweza kuwa umechubuliwa. Raia hawajali kuhusu magari wao magari kuchubuana ni kawaida na sio kesi. Watu wanaweza gongana magari waaishia kusem INSHALLAH. Hao wanasepa hakuna kesi.
Madereva wa Senegal wanapenda kukimbiza sana magari. Sijui wanawahi wapi speed 120 kwao ni kawaida.
UPDATES
17. BIASHARA NA FURSA ZA KIUCHUMI.
Upande wa biashara hawa watu wana ujanja ujanja sana. Kama ni mgeni utapigwa sana kwenye bei. Ukitajiwa bei na machinga wa huku we gawanya kwa mbili ndio muanze kunegotiate. La sivyo utakuwa unalipa hela zaidi....
UPANDE WA PRODUCT
Fursa nyingi nilizoziona hapa ni upande wa kilimo. Sehemu kubwa ya ardhi ya Senegal ni kavu na haistawishi mazao. Vyakula ni bei kiasi. Kila kitu wanapima kwa kilo. Sio chungwa, sio tikiti wala apple vyote utapimiwa kwa kilo.
kilo moja ya parachichi ni XOF 2,500 mpaka 3,000/= ambayo ni kama 10,000/= mpaka 1,2000/=....
Kilo ya chenza ni kama 8,000/= Tshs n.k
Mazao mengi ni imported. Hawalimi sana hawa na pia wanatumia GMO sana.
SEKTA YA UJENZI NA TECHNOLOGIA
Upande wa sekta ya ujenzi ni moto nchi inajengwa sana. Kuanzia material supplying mpaka experts na ma consultant wanahitajika sana....
..........
Fursa za kiuchumi nitaanza ziweka hapa nataka nifanye uchunguzi ili nisiwape matango pori....
17. UTALII.
Upande wa utalii tunaanza na lango la utumwa wenyewe wanapaita kisiwa cha GOREE...
1. GOREE
Hiki ni kisiwa kinachopatikana kilomita 3 kutoka katikati ya Dakar. Kisiwa hiki ndio kilikua lango la kutolea watumwa West Afrika.
Kwa miaka mia 4 kisiwa kilitawaliwa na Wareno, wajerumani, wafaransa, waingereza.
Black American hupenda kwenda hapa kwa ajili ya kujua asili yao na kuomba kwa mababu.
Ni kisiwa chenye historia kali sana.
Pope John paul (Aliomba msamaha hapa)
Mandela
Obama
Bush
Clinton
ni baadhi ya watu mashuhuri kutembelea hapa.
**************************************
Dakar na ombaomba ni kama chanda na pete.
Nikiendelea kukumbuka nitaendelea kujazia kadri ya uwezo maana ni muda umepita tangu nipite pale.