Usiyoyajua kuhusu talaka

Usiyoyajua kuhusu talaka

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
HEBU SOMA AYA HII KATIKA QUR'AN KWA UMAKINI MKUBWA NA KUTAFAKARI...
Suurat At-Talaq 65:1

"يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا۟ ٱلْعِدَّةَۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ رَبَّكُمْۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّآ أَن يَأْتِينَ بِفَٰحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍۚ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُۥۚ لَا تَدْرِى لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا

Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya."

MAELEZO:-
Watu wengi wanaishia tu kuaminishwa kuwa dini yetu imetupa uhuru holela wa kuacha acha(TALAKA) tu unapojisikia ovyo ovyo...

Laa...HAPANA KABISA...HATA KIDOGO...

Dini imetupa ruhusa ya kuachana(TALAKA) pale inapobidi...ILA KUNA TARATIBU ZAKE AMBAZO KILA MUISLAM LAZIMA AZIFUATE AWE MUME(anayeacha) au MKE(anayeachwa) PALE TALAKA INAPOBIDI KUFANYIKA NA PALE INAPOTOKA...

Tukirudi kwenye aya hapo juu...

ALLAAH(Mungu na Mola Mlezi wa ULIMWENGU MZIMA, anayestahiki kuabudiwa pekee yake) Anamuamrisha Nabii wake Muhammad(صلى الله عليه وسلم) PAMOJA NA WAFUASI WAKE(WAISLAM WOTE
, Kuwa mnapokusudia kuwaacha wake zenu(KUTAKA KUMUACHA MKE/ KUMPA TALAKA MKE) Basi Muwaache katika IDDAH/TWAHARA ZAO...

IDDAH/TWAHARA ya MWANAMKE ni kipindi ambacho MKE AMEMALIZA DAMU YAKE YA HEDHI NA TANGU AMEMALIZA DAMU YAKE YA HEDHI HAJAINGILIWA NA MUMEWE...

Na hiyo ndiyo IDDAH/TWAHARA ambao ndio muda ALLAAH AMETUAMRISHA TUWAACHE WAKE ZETU KATIKA HALI HIYO ENDAPO TUKITAKA KUWAACHA(kuwapa Talaka)...

Kwahiyo endapo umechukizwa na mkeo katika kipindi tofauti na hicho alafu ukakusudia Kumpa talaka, BASI KAMA KWELI WEWE NI MUUMINI MCHAMUNGU UNALAZIMIKA KUSUBIRI MPAKA IINGIE IDDAH/TWAHARA YAKE...

Swali: Na je ukimpa talaka mke nje ya kipindi hiko nini kinatokea?
Jibu: TALAKA INAKUWA IMEPITA NDIO, ila MUME ALIYEACHA ANAKUWA AMEPATA DHAMBI KUBWA SANA MBELE YA ALLAAH KUTOKANA NA KUASI KWAKE AMRI YA ALLAAH...

PILI: ALLAAH katika aya hiyo hiyo anaamrisha, ENDAPO MKIWAACHA SASA WAKE ZENU(Iwe vile alivyoamrisha Allaah au kinyume)...BASI MSIWATOE KWENYE NYUMBA ZENU(Yaani msiwafukuze) na wala WAKE ZENU WENYEWE WASIONDOKE KWENYE NYUMBA YAO MPAKA AMALIZE EDA YAKE. (Eda ni VIPINDI VYA DAMU YA HEDHI VITATU)...

Maana yake abaki kwenye nyumba yake hiyo hiyo chini ya mumewe ahudumiwe na mumewe aliyemuacha vilevile alivyokuwa akihudumiwa kabla ya kuachwa...kadri ya uwezo wa mumewe...wala asidhuriwe...
Katika kipindi hiko, MKE ANARUHUSIWA kujipamba kwa ajili ya mumewe ili amvutie na warejeane...

Katika kipindi cha eda MKE NA MUME WALIOACHANA HAWATOLALA CHUMBA KIMOJA...ENDAPO WAKIINGILIANA
TU, BASI INAHESABIKA TALAKA IMEVUNJIKA NA NDOA IMEREJEA KAMA MWANZO...

NA YEYOTE ANAYEMWACHA MKE ALAFU AKAMFUKUZA NYUMBANI KWAKE...AU MKE AKAAMUA KUONDOKA MWENYEWE WAKATI WA EDA...AU MUME AKAMFANYIA VITENDO VYA KUMDHURU MKEWE ILI AONDOKE MWENYEWE...UNAPATA DHAMBI KUBWA SANA MBELE YA ALLAAH...

NA SHERIA HIZO ZIMEWEKEWA EXCEPTION KWA MAKOSA YA UZINIFU, UCHAWI NA UCHAFU MWINGINE MFANOWE...

ALLAAH NI MJUZI ZAIDI...

JE WANGAPI WANAFUATA SHERIA HIYO? JE INGEKUWA WATU WAFUATA SHERIA HIYO...JE TALAKA TALAKA ZINGEKUWEPO?

ALLAAH ANA HEKIMA MNO JUU YA YALE ANAYOTUWEKEA KATIKA SHERIA YETU...YOTE NI KWA FAIDA YETU WENYEWE...

NA SIFA NJEMA ZOTE NI ZAKE ALLAAH MOLA WA ULIMWENGU WOTE...

NAKARIBISHA MASWALI INSHAA ALLAAH...
 
Sheria za nchi hii zinatambua kuwa chombo Cheney mamlaka ya kuvunja ndoa ni mahakama tuu
 
Nilitaka kuona kama talaka imepigwa marufuku. Nimeelewa kua ipo ila kuna mchakato wa kushughulika nao.
 
Kwahiyo mkuu umeskia sisi ote ni wahindi?
Hivi ada ulitulipia wewe
Aisee sio kila post uionayo kwenye display ya simu yako inahitaji comment yako...

Zingine unasoma unapita hivi...acha ulimbukeni...
 
Aisee sio kila post uionayo kwenye display ya simu yako inahitaji comment yako...

Zingine unasoma unapita hivi...acha ulimbukeni...
Ungeweka wazi kuwa post hiyo ni kwa waislam ieleweke maana umechanganya na kiarabu
Usituchanganye nasoma popote ninapotaka
 
TALAKA INAKUWA IMEPITA NDIO, ila MUME ALIYEACHA ANAKUWA AMEPATA DHAMBI KUBWA SANA MBELE YA ALLAAH KUTOKANA NA KUASI KWAKE AMRI YA ALLAAH.
Hii kauli mimi sikubaliani nayo.

Kutoa talaka wakati wa hedhi ni bidaa.

Na hakuna bidaa inayokubalika kwa kauli ya Mtume كل بدعة ضلالة
Kila bidaa ni upotevu.

Na katika kauli nyingine ya mama aisha kutoka kwa rasul "atakayetenda tendo ambalo halina amri yetu basi atarudishiwa nalo mwenyewe"

Sasa hakuna amri ya Mtume inayosema kuwa tutoe talaka wakati wa hedhi,kitendo hicho hakikubaliwi.

Japokuwa zipo khilaaf za ulamaa ila mi naona kauli yenye nguvu na mantiki ni ile ya kuwa talaka haipiti.

Wewe ndugu yangu una maoni gani katika hilo ?
 
Back
Top Bottom