Kiuchumi. hali ya maisha kwa sasa ni ngumu sana, kijana wa miaka 21 lazima atakuwa chuo au katika miaka yake ya mwanzo kazini. Hapo kumpa mzigo wa kuoa ni kuongeza mzigo kwa taifa.
Si kweli maneno yako, maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua, uko unapotaka wewe aelekee ndio kwenye maangamizi makubwa sana, na ndio kwenye matumizi mengi ambayo angeweza kuyaepuka.
Unapomfata mwanamke ili ukazini naye, mara nyingi tumeshuhudia matumizi mengi ili kuonyesha kuwa wewe unazo na mwanamke akupende. Mtakwenda Guest House, mtakunywa na kula na pesa utampa.
Lakini kama ni mkeo, nyumba unayoishi ndio atakayoishi, chakula utakacho kula ndio atakacho kula, na wakati mwingine mke anaweza kuwa naye ni mfanyakazi, na si lazima ategemee kila kitu toka kwa mume, kwa ufupi watasaidiana maisha.
Kijamii, jamii inamtegemea kijana kwa ulinzi na uzalishaji mali, kwa umri huu kuoa ni kuondoa attention kwa jukumu hili kwa jamii na kuhamishia kwa mke.
Jamii inawaamini sana wanaume wenye majukumu na haswa wale walio owa, hata heshima yake itaongezeka. Mwanaume anapooa, uachana na mambo yote ya kupoteza wakati na hata makazini wanakuwa ni wachapakazi hodari na kwa sababu anajuwa kuwa ana mtu nyumbani ambaye anamtegemea, kwa hiyo hafanyi mchezo na wala hawi mzembe.
Kisiasa, huu ni umri wa harakati na kujitoa, kijna akiwa na mke ita compromise ushiriki wake( angalia, zitto,mnyika, sugu, wote hawajaoa ndio maana wanaweza kuthubutu)
Kisiasa walio owa ni watu makini sana kwa sababu kama unashindwa kuongoza nyumba yenye mke mmoja labda na mtoto mmoja ama wawili, basi vipi tukupe jukumu la luongoza maelfu ya watu. Tunasema kama wewe ni mtu bora nyumbani kwako basi utakuwa vilevile bora kwa jamii.
Hao uliowataja hapo, ebu angalia maamuzi yao na ushirika wao kisiasa, bila kuingiza ushabiki theni utatambua wamesimamia wapi.
Kimazingira, mke ina maana kijana pia ataanzisha familia yake tofauti na ile ya wazazi wake that means matumizi zaidi ya nishati, na uzalishaji wa uchafu, kupunguza uharibifu wa mazingira ni bora vijana wachelewe kuoa.
Hii kwa kiingereza ndio tunaita Covetousness, Avarice, greediness.
Unasema kuwa vijana ni vema kuacha kuoa, kwa maana waendelee uzinifu na wanawake watabebeshwa mimba na kuzaa watoto watakao lelewa bila baba zao, na ili ni janga kubwa sana kwa dunia hii ya leo.
Naam, wachumi wa Kimagharibi ndio walikuwa na mawazo hao, na ili walilipigia sana debe kwenye nchi zao, na matokeo yake ikapatikana gape kubwa sana kati ya vijana na wazee, hivi sasa wanasisitiza wananchi wao wazaane kwa sababu wageni kutoka nje ndio wenye kushika atamu kwenye nyanja za uzalishaji mali.
Kwa nini tukimbilie dhana ya upunguzaji wa watu na hatuikimbilii dhana ya kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma za kijamii?
Kwa nini tusiikimbilie dhana chanya ya uongezaji wa uzalishaji, dhana ambayo itatusukuma kuongeza nguvu kazi za makusudi ili kukuza hali ya uchumi?
Rasilimali ya kututosha sisi leo na hao watakaokuja kesho tayari ipo, kinachohitajika tu ni nguvu kazi iambatanayo na juhudi, maarifa na matumizi sahihi ya rasilimali hiyo, sambamba na kuilinda kwa faida yetu na faida ya vizazi vijavyo.