Katika pita pita zangu mchana wa leo jiji Dar es Salaam,
Nimekutana na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila katika ofisi fulani, yeye kaja na yake, nami na yangu hivyo tukaa waiting room pamoja kumsubiria mwenyeji wetu.
huwezi amini alinichangamkia sana na tukaanza kuchat.
Kwanza nilimuuliza kwa nini wapinzani hawaungani?.
Jamaa alishusha nondo nzito kwa kubonda wapinzani wote kuwa Tanzania, hakuna mpinzani yoyote isipokuwa ni yeye tuu!, tena kuhusu Chadema, ndio usiseme kabisa, eti ni afadhali ya CCM!. Alisema mengi kwa lugha kali na matukano kibao, huku akizungumza kwa sauti ya juu, ofisini kwa watu!.
Nikamsisitizia, kwa vile chama tawala ni CCM, vingine vyote ni upinzani, jee haoni kuikandia Chadema na CUF at this time ya kuelekea uchaguzi mkuu ni kuikampenia CCM kwa mlango wa nyuma?, au ameshikishwa kidogo dogo?!.
Jamaa aliwaka sana akasema CCM imshikishe nani pesa, hapa nilipo, japo sina pesa ila nimekataa hongo ya milioni 100! toka kwa ....(akamtaja jina....) naomba nilihifadhi ili kuilinda hadhi ya JF, maana huyu mtu kwa JF, ni "mtakatifu fulani" sana humu jf, na ni mmoja wa waheshimiwa wetu kitaifa, hivyo anaheshimiwa sana tuu humu jf!
"Niligundua kuwa ... (akamtaja) ni muuaji, anatoa pesa kutuma assasins kutekeleza mauaji mbali mbali na kisha kufake accidents!, alitoa shilingi milioni 120 kuwapa Wakenya fulani wawili kumuua ...(akamtaja..), ushahidi ninao!.
Mtikila akaendelea kudai kuwa, Mfanyabiashara huyo tajiri alipomgundua siri yake ya mauaji imefichuka, kwanza alimuita kwenye(Mtikila) kwenye moja ya vitega uchumi vyake (akataja siku, muda na mahali) akampa offer ya hongo ya Sh. Millioni 10 ili afute jina lake kwenye dossier ya wauaji. Mtikila akamkatalia.( Akimaanisha analo andiko hilo la mauaji!).
Mara ya pili (tajiri) huyo alimuita ofisini kwake, (akataja siku, muda na osisi ilipo!) akapanda dau toka ile milioni 10! mpaka milioni 50!, bado Mtikila alizikataa!. Ndipo tajiri huyo akamuita Mtikila nyumbani kwake (akataja siku, muda na eneo nyumba ilipo!) akampa offer ya Sh. Millioni 100!. Ndipo Mtikila alimkubalia kwa shurti ya tajiri huyo, kwanza ampigie magoti yeye Mtikila na akiri dhambi zake, na pili atubu kwa Mungu, Mungu akishamsamehe ndipo yeye Mtikila, ataipokea hiyo pesa kama asante yake!.
.
Tajiri akagoma kukiri na akagoma kutubu!. Ndipo Mtikila akasimama akatoka nje!, ila anadai kila kitu amerekodi kwenye digital sound recorder yake, na sasa anasubiri tuu time muafaka ili amlipue!.
Na baada ya maelezo yote haya ya kukataa hongo ya milioni 100!, Mchungaji Mtikila alimalizia kwa ...(nakihifadhi)
Pasco