Uso wenye mafuta mengi; Ushauri mafuta gani nitumie?

ZENITH

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
1,035
Reaction score
920
Kama title inavyojieleza,marafiki mwenzenu nina shida kubwa ya mafuta mengi usoni,kila mafuta ninayotumia yanagonga mwamba kiasi kwamba nimeamua kutotumia mafuta yoyote yale ili kuepukana na tatizo la pimples.

Umri wangu ni mkubwa tu(30yrs) but bado nikipaka mafuta kama nivea for men,rapid white 21 jours,vaseline men body lotion,HOBBY na mengineyo mengi tu lakini yoote hayo yote nimepiga mbizi kwenye kokoto.Wengi watanishauri kwenda SH HARMONY lakini kama kuna njia mbadala naombeni msaada wakuu,thanks in advance!
 
Tumia vitu vya asili vya kupunguza mafuta kama Limao changanya na ute wa yai, au tumia product za tea tree zinasaidia pia
 
sh hamon wahun tu nilishawahi kwenda pale kwa tatizo kama hilo lakn walinifungia makorokoro ya elf 50 lakn kutumia chunus palepale
 
SH hao wanamafuta ya kawaida sana na gharama juu mkuu pole kwa tatizo subiri wadau waje .... Binafsi sijawah tumia lotion ni mwendo wa gando tu
 
Tafuta kitu kinaitwa "clean and clear"---facial wash. Ni maarufu ya kuoshea uso. Haina sabuni. Hakikisha unaosha uso wako kila mara upatapo nafasi kwa hiyo kitu. Ukioga kabisa malizia kunawa uso kwa hiyo kitu. Acha kupaka mafuta au lotion kabisa. Utajiona uso umepauka lakini ukikaa kidlgo tu utaona uso utakuwa vizuri tu. Mimi nilikjea na chunusi zaidi ya cheaping za ukuta! Kwasasa sina hata moja. Uso bado unamafuta ila nimeacha kupaka mafuta wala lotion.
 
Ata mimi nna tatizo hilo ila niambiwa nitumie saban za alvera na nisipake mafta yoyote usoni.
 
Kama title inavyojieleza,marafiki mwenzenu nina shida kubwa ya mafuta mengi usoni,kila mafuta ninayotumia yanagonga mwamba kiasi kwamba nimeamua kutotumia mafuta yoyote yale ili kuepukana na tatizo la pimples.
Umri wangu ni mkubwa tu(30yrs) but bado nikipaka mafuta kama nivea for men,rapid white 21 jours,vaseline men body lotion,HOBBY na mengineyo mengi tu lakini yoote hayo yote nimepiga mbizi kwenye kokoto.Wengi watanishauri kwenda SH HARMONY lakini kama kuna njia mbadala naombeni msaada wakuu,thanks in advance!

Polesn kwa tatizo ila sasa utafurahi. Tafuta asali uichemshe kidogo na tango ulilolisaga. Baada ya sekunde chache epua, acha ipoe. Kisha paka usoni iache kwa muda wowote haina madhara ukichoka toa nawa uso wako. Asubuhi kuwa na tabia ya kunywa maji yenye uvuguvugu kwa mbali km lita hivi lkn uchanganye na asali ni dawa pia. Pamoja na hayo kiujumla penda kunywa maji mengi.
Ni dawa ya asili haina madhara yoyote na haina cha kuchagua ngozi wala nini.

Achana kbs na mambo ya lotion sijui cream. Utafurahi kwa muda ila itabidi uwe mtumwa wa hivyo vitu muda wote.
 
Tafuta kitu kinaitwa "clean and clear"---facial wash. Ni maarufu ya kuoshea uso. Haina sabuni. Hakikisha unaosha uso wako kila mara upatapo nafasi kwa hiyo kitu. Ukioga kabisa malizia kunawa uso kwa hiyo kitu. Acha kupaka mafuta au lotion kabisa. Utajiona uso umepauka lakini ukikaa kidlgo tu utaona uso utakuwa vizuri tu. Mimi nilikjea na chunusi zaidi ya cheaping za ukuta! Kwasasa sina hata moja. Uso bado unamafuta ila nimeacha kupaka mafuta wala lotion.

Shukrani mkuu kwa mchango wako, nitaufanyia kazi.
 
Jamani! hivi kuwa na mafuta mengi usoni ni yatizo?Mimi naona kama yale uliyokula mwili ume preserve vipi iwe tatizo.kuna wale wanaokuwa na ukavu ngozi hilo naona ndo tatizo.Ina maana kwao mafuta ni under rate.
 
ila mkuu nadhani tatizo lipo ndani ya damu hata ukitumia lotion nje ya ngozi bado effect itaonekana
unaonaje ukaenda kwa wataalamu wa ngozi mahospital na sio kwenye vipodozi
 
Tafuta Baking Soda Na Uandae Uji mzito Upake Uso Kaa Nao Kwa Dak 5
Nimesoma mahali Kuwa baking soda ni alkaline so INA disturb PH ya USO inaifanya ngozi I we rahisi kushambuliwa na vt kama chunusi
 
Polesn kwa tatizo ila sasa utafurahi. Tafuta asali uichemshe kidogo na tango ulilolisaga. Baada ya sekunde chache epua, acha ipoe. Kisha paka usoni iache kwa muda wowote haina madhara ukichoka toa nawa uso wako. Asubuhi kuwa na tabia ya kunywa maji yenye uvuguvugu kwa mbali km lita hivi lkn uchanganye na asali ni dawa pia. Pamoja na hayo kiujumla penda kunywa maji mengi.
Ni dawa ya asili haina madhara yoyote na haina cha kuchagua ngozi wala nini.

Achana kbs na mambo ya lotion sijui cream. Utafurahi kwa muda ila itabidi uwe mtumwa wa hivyo vitu muda wote.
zingatia huu ushauri mm mwenyew shuhuda ,,
 
Back
Top Bottom