SoC02 Usomaji vitabu ni tunu, usipuuzwe

SoC02 Usomaji vitabu ni tunu, usipuuzwe

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 29, 2022
Posts
16
Reaction score
15
Maana ya Vitabu.

Neno kitabu/vitabu huweza kumaanisha maandishi yaliyoandikwa kwa mkono au mashine au kupigwa chapa katika kitu chochote na yakafunganishwa au kuwekwa kwa taratibu Fulani. Kitabu kina uwezo wa kuwa katika ukubwa wowote kutoka kurasa kumi hadi maelefu.(Mbena : 1972,1).ikumbukwe ya kuwa usomaji wa vitabu waeza kuwa kwa lengo la kujistarehesha au kupata elimu juu ya mabo flani.

Usomaji wa vitabu nchini Tanzania na afrika kiujumla, umekuwa ukichukuliwa kwa mtazamo hasi;usomaji wa vitabu ni wa wazungu tu, au wasomi. Huu mtazamo umechochea kudumaza usomaji wa vitabu kwa watu wengi hususani hata kwa hao wasomi wenyewe. Kwa miongo kadhaa iliyopita ilikuwa ngumu huu utamaduni kukua labda yawezekana na watu wengi kutojua kusoma na kuandika,lakini pia upatikanaji wa vitabu .

Lakini kutokana na maendeleo na ukuaji wa sayansi na teknolojia upatikanaji wa vitabu umekuwa ni rahisi sana ,ingawa cha kusikitisha ni kuwa ,usomaji wa vitabu unadhidi dorola kwa kiwango kikubwa,sio wanafunzi,wasomi,na jamii kiujumla. Kuna website NA Apps mbalimbali zinazotoa fursa ya kupakua vitabu bila gharama yoyote na vitabu vingine kwa gharama nafuu: kwa mfano “Amazon,Light Reader, Pdf drive” na nyinginezo zinazopatika katika ‘’Google na play Store’’ . Lakini pia, kuna makundi tofauti tofauti ya” whatsapp yanayojihusisha na usomaji wa vitabu,ambapo vitabu mbalimbali huwekwa humo ili uweze kujisomea.

Upuuzaji wa usomaji vitabu, umechangia sana kuwa na “wasomi kasuku”;wasomi wasioweza hata kuzalisha nadharia mbalimbali,nadharia ambazo zingeweza kuwa chachu ya maarifa,ujuzi na ubunifu wenye tija kwa jamii zetu za kiafrika na ulimwengu kiujumla.

Sio ajabu katika kizazi hiki, kumkuta “msomi” mwenye shahada yoyote ya elimu,lakini hajui hata majina matano(5) ya vitabu vitano na waandishi wake katika fani aliyosomea. Swali la kujiuliza ,je, kama msomi huyo ameshindwa kujua majina ya vitabu vya fani au kozi anayosomea, atawezaje kujua na kusoma vitabu nje ya fani aliyosomea? ,jibu ni fupi kuwa huyo “msomi” hatasoma vitabu . lakini, tushiishie hapo lazima tuanzishe,tuendeleze na kukuza utamaduni wa kujisomea kwa jamii zetu ili kuwa na kizazi chenye maono pevu,chokozi,maarifa ya kutosha na ubunifu yakinifu.

UMUHIMU WA KUSOMA VITABU

Hivyo basi,najua unaweza kujiuliza kuwa kuna umuhimu gani utokanao na usomaji wa vitabu.hivyo wacha niangazie kwa kifupi, umuhimu wa kuanzisha, kukuza na kuendeleza utamaduni wa usomaji wa vitabu kwa jamii zetu kwaajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na baadae;

Mosi, usomaji wa vitabu humpatia msomaji maarifa,ujuzi na uzoefu wa maisha ya ulimwenguni. Kama msemo wa wahenga usemavyo,” mtembea kwingi,kaona mengi”, vilevile , mtu aliye na mazoea na utamaduni wa kujisomea huwa anakuwa na maarifa , ujuzi na uzoefu wa kutosha katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi ,kisiasa na kiteknolojia. Hii huchagizwa na hoja ya kuwa msomaji wa vitabu huwasiliana moja kwa moja na mwandishi husika kupitia mandishi na alama zipatikanazo katika vitabu. Kwa mfano, pindi usomapo kitabu cha Ben Carson,Yeriko nyerere,Kwame,shabaan Robert,Robert Kiyosaki,Donald Trump,Chimamanda Ngozi Adichie,Chinua Achebe na wengine wengi ,lazima upate maarifa,ujuzi na uzoefu wa yale waliyoyapitia maishani mwao,na shauku zao.

Pia,usomaji wa vitabu humpatia msomaji mawazo na njia mpya za maisha(kumbadilisha mitazamo na misimamo/itikadi). Mara nyingi binadamu huwa tunaishi kutokana na mazoea ya mazingira na malezi tuliyolelewa,lakini wakati huohuo jinsi tunavyoishi,amini na mitazamo juu ya mambo kadha huwa tunakuwa tumeathiriwa hasi au chanya. Hivyo vitabu hukupatia ukurasa wa kuyatazama maisha katika kona tofauti na uliyoizoea au kunoa mawazo yetu kuhusu maisha. Kwa mfano, nani aliweza taraji mtu aliyekuwa kibaka,muuza madawa ya kulevya,mwizi,mcheza kamari na mtu asiye na elimu yoyote ya chuo ,kuwa atakuja kubadilika na kuja kuwa mtu bora,mwanaharakati wa haki za binadamu/watu weusi,na mtu mwenye ushawishi mkubwa duniani? Sio rahisi katika hilo,lakini usomaji wa vitabu (akiwa gerezani ) ,ulibadili njia,mitazamo na imani juu ya maisha aliyokuwa akiyaishi awali hadi kuja kuwa mtu muhimu ulimwenguni.

Kama ilivyo chakula kwa mwanadamu,vivyo hivyo usomaji wa vitabu ndio moja ya chakula muhimu kwa ubongo wa mwanadamu; ukihitaji fikra na uwezo wako wa kufikiri kunoreka,basi usomaji wa vitabu ndio tupa(kinoleo) bora kabisa. Jaribu kufikiri,watu kama akina Maxence Melo anawezeje kumiliki na kuongoza mtandao kama Jamii Jorum miaka nenda rudi jukwaa kama hili? ,Fikiri pia msanii kama; Farid kubanda ali maarufu Fid q,Nash Mcee,Dizasta na wengine wengi wanawezaje kuandika nyimbo; zenye jumbe nzito na suluhu nzito za maisha kiwango cha juu? Jibu ni fupi tu, kuwa bila shaka hao watu ni wasomaji wazuri wa vitabu.

Uwezo wa kuzungumza vyema na kushawishi mbele za umma (hadhira) huchagizwa na usomaji mzuri wa vitabu. Hii huchochewa na sababu kubwa kadha; uwezo wa kujenga hoja na mpangilio wa kile unacholenga kukizungumza. Mambo yote hayo huambatana na usomaji wa vitabu. Mtu kama profesa Patrick Otieno Lumumba,Malcom X,Barack Obama,Leo Muhamad,Haris Kapiga n.k wanawezaje kuzungumza mambo mbalimbali bila kumchosha msikilizaji?, elewa kuwa hao jamaa ni wasomaji wazuri wa vitabu.

Kwa kuongezea,usomaji wa vitabu ndio nyenzo ya uandishi bora . elewa kuwa mwandishi bora yoyote ni zao la uysomaji mzuri wa vitabu,makala,na majariida mbalimbali yapatikanayo mtandaoni au sehemu yoyote. Mtu kama Ben Carson,Chimamanda ngozi Adichie,Chinua,Chinua Achebe,Robert Kiyosaki,Donald Trump,Wole Soyinka na wengine wengi wamekuwa ni moja ya zao la wasomaji wazuri wa vitabu.

NINI KIFANYIKE KUANZISHA,KUKUZA, NA KUENDELEZA UTAMADUNI WA USOMAJI WA VITABU.

Ningetoa rai kwa raia kwa Serikali, taasisi binafsi, asasi za kiraia, na mtu mmoja mmoja waongeze nguvu kuhamasisha utamaduni wa usomaji mzuri wa vitabu. Lakini pia, ningependekeza, maktaba ziongezwe;ikiwezekana kila wilaya na kata ziwe na maktaba, ili kuwezesha usomaji wa vitabu kukua.

USOMAJI WA VITABU NI TUNU;UWEZESHE,UTUNZWE NA KUENDELEZWA.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom