Miaka mingi inapita na kila ripoti ya CAG inaposomwa inabainisha kiasi kikubwa cha fedha kinachopotea au kutumika kwa ubadhirifu. Mfano, sehemu ya ripoti ya mwaka 2021/2022 imebaini mianya ya uvujaji wa mapato ambapo bilioni 17 hazikuweka benki.
(Niliyoyashudia eneo langu) katika matumizi ya “POS” mkusanya ushuru kati ya halmashauri mojawapo alikuwa anadai zaidi miezi 6 ambayo hakulipwa ujira wake lakini yeye mwenyewe kupitia hiyo pos alikuwa anajua jinsi alivyokuwa anazalisha ziada yake na ile kidogo ya kupeleka halmashauri huku akitaja changamoto nyingine inayomkabili ni ukosefu wa uwiano sahihi kati ya fedha anazodaiwa kwenye mfumo huo na risiti alizotoa kupitia pos kwani ni tofauti.
Kupitia mfano huu ni dhahiri shairi kwamba mianya ya “rushwa na ubadhirifu”inatengenezwa na mamlaka husika pale zinaposhindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha mazingira ni shawishi kwa ubadhirifu wa fedha za umma.
Sababu nyingine ya kukosa suruhisho la ubadhirifu huu ni kukosekana kwa taasisi yenye kuwawajibisha "kiutendaji" wale wote wanao husika na ubadhirifu huu hiwe ni mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu au taasisi zinazoisababishia serikali hasara kubwa ya kupoteza mabilioni ya fedha na pengine uwajibishaji ukifanyika unawagusa watu wa ngazi ya chini na kuwaacha “mapapa” wanaoruhusu mianya hii.
Katika kutafuta suluhu ya kudhibiti ubadhirifu huu:
Ningependekeza uanzishaji wa ripoti ya "WAJIBISHO LA RIPOTI YA CAG"
Wajibisho la ripoti ya CAG nini?
Hii hiwe ni usomaji/ au utohaji tu wa orodha ya watu na taasisi zilizofanya ubadhirifu wa fedha za umma mbele ya vyombo vya habari na kutamka wazi wazi watu hao wamewajibishwa kwa adhabu gani kulingana na sheria za nchi.
Au
Wao wenyewe wamewajibikaje kulingana na ubadhirifu waliofanywa.
Sababu ripoti ya awali inaposomwa watu wanakaa kwenye mijadala ya fedha zilizopotea kuwa ni nyingi kuliko kuyafanyia kazi mapendekezo ya CAG na kufatilia hatua zilizochukuliwa, yaani “ripoti inamezwa na ubadhirifu kuliko jinsi gani ubadhirifu huo unavyopaswa kutokomezwa na jinsi ya kuiziba mianya hiyo”.
"Wajibisho la CAG" liwe linasomwa kabla ya ripoti ya CAG ndani ya mwaka husika, hii itachochea kuupunguza ubadhirifu kwenye ripoti itakayofuata na kuonyesha uwajibikaji wa mamlaka hii chunguzi na kuendelea kuipa nguvu ya kiutendaji.
Yaani ofisi ya mkaguzi Mkuu wa serikali iwe na utaratibu wa kutoa taarifa mbili "ripoti mbili", taarifa ya kwanza hiwe ni "Wajibisho la ripoti ya CAG" kwa kueleza hatua zilizochukuliwa "adhabu" na kiasi kilichorudishwa au kilichonusuriwa" kutoka kwenye mikono ya wabadhirifu ndani ya ripoti iliyopita na taarifa ya pili iwe ni ripoti ya CAG ndani ya mwaka husika.
Ripoti uandikwa baada ya uchunguzi wa kina hivyo sina mashaka kuwa taarifa zinazosomwa na mkaguzi mkuu wa serikali kuwa niza kubumba bila ya kufanyiwa uchunguzi, kama kizingiti cha kupata suruhisho la ubadhirifu huu ni kukosa nguvu ya kuwawajibisha kutoka kwenye ofisi hii ya mkaguzi mkuu wa serikali basi mamlaka zenye nguvu hiyo zipokee taarifa ya mkaguzi mkuu, ziifanyie kazi "Wajibisho la kimamlaka " kisha zitoe mrejesho kwa mkaguzi mkuu ili aweze kuonyesha matunda ya ripoti yake pale atakapokuwa anasoma "WAJIBISHO LA RIPOTI YA CAG" mbele ya vyombo vya habari au bunge.
Rai yangu kwa Serikali chini ya Rais pamoja na bunge wasikubali kusomwa na kupokea ripoti mpya ya mwaka husika bila kuliona "wajibisho la CAG" yaani wajibisho la ripoti iliyopita.
Kasumba ya kusoma tu ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali bila kuonyesha adhabu na hatua sahihi kwa wabadhirifu ni kichochezi kikubwa kinachosababisha tuendelea kuona madudu yanayokosa suruhisho.
Hii hapa chini ni moja ya kazi niliyoiandaa mwaka 2022 baada ya kusikia kilio cha mmoja wa wakusanya mapato huku nikitafakari lipi liwe suruhisho....
TUNAMEZWA VIDAGAA.
Tunavuliwa na rangi, hayataki tukakue
Domo zao hayafungi, yatumeza yatuue
Ziwani tunayomengi, wajuani yasikie
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa
Majini yanapakato, yanazichezesha kasa
Hayoni tunawatoto, makubwa yatunyanyasa
Madogo yanachecheto, sirini yana darasa
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa.
Ni mavuvi ya kisasa, mataya yanapanua
Yakishiba yananesa, madili yamepungua
Hakuna wa kuyagusa, uwoga watusumbua
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa.
Sio tu ziwani nyasa, tangayika Victoria
Na ipo mingi mikasa, teso zidi malaria
Tumbo zao yapapasa, yakishiba yabeua
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa.
Wafikapo watalii, vidagaa twaonewa
Kwa kuwa sisi watii, lawama tunatupiwa
Twaonekana adui, vidagaa twachukiwa
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa.
Nani wakututetea, nasi tusije potea
Uonevu ukikua, majini tutaishia
Japo wajanja dagaa, nao wanajishibia
Kuyashibisha mapapa, tunamezwa vidagaa.
Myororo sendelee, uje sumeno makata
Mizizi ututolee, haifai kata kata
Shina zisichepukie, kwendelea kukamata
Tunamezwa vidagaa, kuyashibisha mapapa.
Nilipoyaona haya nikafikiri suluhu yake ni mshororo huu
“Myororo sendelee, uje sumeno makata”
Basi huu msumeno makata huwe ni WAJIBISHO LA RIPOTI YA CAG.
Kupitia usomaji wa ripoti hii pendekezwa ya "WAJIBISHO LA RIPOTI YA CAG" kutamakinisha viongozi na watendaji wengine kwani hakuna atakaye kosa umakini wa kufuata sheria na miongozo katika majukumu yake baada ya kuona wanaotenda madudu wanawajibishwa ipasavyo.

Upvote
2