Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,925
Ni juzijuzi hapa ambapo tumeshudia Rais wa China akiongea kwa lugha yake, wakati Rais wetu anaongea Kiingereza. Hotuba hizo zilifaa wananchi wote wazielewe kupitia lugha yao ya Kiswahili. Viongozi wengi wanachanganya Kiswahili na Kiingereza wakiongea na wananchi, na vile vile televisheni zetu pia zinarusha habari watu wanaongea Kiingereza bila kuweka maneno ya kutafsiri. Mitaani kwetu napo limekuwa jambo la sifa kusikika mtu anachanganya lugha hizo, eti ni kuonekana kuwa ameendelea au amesoma! Tatizo ni kuwa wengi ambao wanaochanganya lugha hizo hawazijui zote vizuri. Ili uweze kuwa mjuzi wa lugha fulani inabidi uweze kuongea lugha kwa ufasaha.
Mwandishi Freddy Macha naye pia ana usongo kama wangu. Soma zaidi hapa:
MAKALA ZANGU: USONGO WANGU NA KISWANGLISHI : WATANZANIA HATUJAKOMAA KILUGHA- 1
Mwandishi Freddy Macha naye pia ana usongo kama wangu. Soma zaidi hapa:
MAKALA ZANGU: USONGO WANGU NA KISWANGLISHI : WATANZANIA HATUJAKOMAA KILUGHA- 1