Ninachobashiri na ambacho ninakiamin kwa dhati kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini ni kwamba ikiwa CHENGE atapata USPIKA basi huo ndio utakuwa ndio wa mwisho wa CCM.
Ni ajabu kuwa CCM inaendelea kufanya makosa makubwa kwa kuwateua watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi. CHENGE ana tuhuma nyingi na mbili ni kubwa. Ya kwanza ni ile ya RADAR na ya pili ni ile ua kusababisha vifo kwa wasichana wawili waliokuwa kwenye Bajaj.
Kwamba CHENGE ameamua kuchukua fomu ya USPIKA ni mkakati ulioandaliwa wa kuwasafisha wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ikiwa ni kinga kwao kwani hawajui nini kitatokea baadaye kuhusu masuala ya EPA, RICHMOND kwani haya hayajaisha.
Kwa ujumla wake siku Tanzania itakavyoachia madaraka huo ndio utakuwa mwisho wa kile kinachoitwa AMANI katika nchi yetu.