Sisi watanzania ni jadi yetu kusaidiana na kukwamuana mtu wako wa karibu anapokuwa na changamoto hasa za kifedha.
Unapomuomba mtu akukopeshe pesa hakikisha unaporejesha unazingatia kuweka gharama za makato aliyotumia wakati wa kukutumia na anapopokea hiyo pesa yaani wakati anatuma na pale atakapoitoa ile pesa.
Kwa lugha nyepesi hakikisha anapotoa hiyo hela iwe kwa bank au Simu anapata pesa yake kamili pasipo upungufu wa hata senti moja.
Unapokopeshwa sio kwamba huyo mtu hana matumizi na hiyo pesa au ana ya ziada, bali amehairisha matumizi yake kwa kuthamini uhitaji ulionao kwa wakati huo.
Ni jambo dogo lakini linadhihirisha ustaarabu wa mtu na nidhamu yake ya kifedha.
Ciao