Nimekuwa mkazi wa Dar kwa muda mrefu na nimekuwa nikishuhudia vipindi mbalimbali vya maisha ya wakazi wake kwa namna ya pekee. Tabia za wananchi hawa au wakazi wa Dar hazitabiliki kiasi cha kushindwa kujua mkazi huyu ata'behave' vipi katika matukio mbalimbali.
Kwa mfano, utaona mkazi huyo akifika kwenye mashine ya kuchukua fedha yaani ATM, atapanga foleni na zamu yake ikifika anaingiza kadi yake na kuendelea na shughuli yake pale. Hapa amekuwa mstaarabu kamili. Lakini huyu huyu mkazi akiwa anaendesha gari na kama kuna kafoleni kadogo basi utamwona anachepuka na kuanza kula service road ili yeye awahi, kana kwamba wale wote aliowakuta kwenye foleni hawana haraka labda au hawajui kutumia magari yao vizuri. Na kwa kitendo chake hicho anaweza akasababisha foleni kubwa zaidi. Hapa ustaarabu wote aliouonyesha kwenye ATM anauvua kabisa. Mkazi huyo huyo atanunua chungwa, akimaliza asitafute sehemu ya kutupia takataka, atatupa ganda la chungwa barabarani, tena sehemu ambayo ni wazi, imesafishwa na wafanya kazi ambao hulipwa kwa ajili hiyo ili kuweka mji, hususani barabara zetu katika hali ya usafi. kwanini ustaarabu wa mkazi huyu hautabiriki? Hapa ana'behave' hivi, pale anakuwa tofauti kabisa kiasi cha kuleta usumbufu kwa wengine??