Ustadh Mganga ambaye ni bingwa wa utabiri hapa Afrika Mashariki ametabiri kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ataanza kupokea tuzo za kimataifa kutokana na kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya hasa katika nyanja za amani,demokrasia na utawala bora,pamoja na mapambano dhidi ya umaskini.
Hili ni jambo jema kwani Jumuiya ya kimataifa imetambua kazi kubwa inayofanywa na Rais huyo wa awamu ya sita.