Ustaarabu wa namna hiyo uliondoka na watu wa kizazi cha mwalimu, ulikuwepo. Kuurudisha sasa itakuwa ngumu sana, ama itatugharimu. Unajua hata mimi nilishangaa sana hapa ofisini kwangu hivi majuzi (niko nje ya nchi), katibu muhtasi akatuma email kwa kila mtumishi, kuwa kama kuna mtu kadondosha noti 'garage' (noti husika ilikuwa ina thamani kama elfu 20 za madafu) aende akachukue kwake. Hiki ni kitu cha kawaida sana hapa mahali, lakini sio uswazi. Hata kanisanani ama msikitini, nina uhakika ukidondosha noti watu hawakurejeshei, wanasunda chini.