jozee jose
Member
- Sep 22, 2022
- 52
- 120
Watasha walisema unachopanda ndicho utakachovuna huwezi panda mihogo ukavuna miwa...
Hivi tulivyo sasa yaani kimawazo, kihisia, kiutendaji na hata namna ya kuyachukulia mazingira ni matokeo ya kile tulichopata kutoka kwa Wazazi wetu au walezi wetu na jamii kwa ujumla.
Sisemi kwamba tuwalaumu wazazi au walezi waliotulea BIG NO , wao walitulea kwa upeo wao wakajitahidi kutuweka kwenye misingi hasa walijikita kwenye maadili ya kiafrika japokuwa walikutana na ukinzani wa utandawazi ambao ni changamoto hata hivi leo.
Sasa tuje kwenye familia za leo ambazo baba na mama wote ni wafanyakazi au tuseme wote wanatafuta ulaji mbali na makazi yao na mwisho wa siku wanarudi jioni. Tutegemee ya kwamba huenda familia kama hii lazima itakuwa na mlezi wa watoto wao wadogo hapo nyumbani kwao. Mlezi anaweza akawa ni sibling/ ndugu au wale wa kulipwa(house made/house girl).
Sasa nini tutegemee kutokea hapa?
Kwanza, Watoto wanaweza wakapata ujazo CHUKI /UHARIBIFU kutoka kwa hao wanaowasimamia na kwa sababu hautakuwa karibu nao kwa ubize uliopo familia zinajukuta zina watoto wajeuri, wabishi, wavivu, wakaidi, Wajuaji,Wakorofi, Wadokozi na nk.
Pili, Watoto watakosa Muunganiko kwenye ubongo wao pia watapata hitirafu kwenye hisia zao hili litapelekea hata wakiwa wakubwa wanaweza wasijali wazazi wao wakiwa hawajiwezi yaani wazee .
Sasa nini cha kufanya?
Kupitia Sikukuu ya Wanawake kuna jambo la kujifunza kidogo, Wanawake watambue ya kwamba wanajukumu zito la uangalizi na malezi ya watoto wao haijalishi wapo kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi ,kisiasa, kidini na nk.
Mfumo wa mwanamke kuwa mlezi wa watoto nyumbani ni mfumo ambao upo kwenye Sheria ya Asili na Sheria ya Asili ni Chembe chembe za Sheria ya Mungu , hivyo basi Malezi bora ili tuwe na kizazi bora, Taifa bora basi tuangalie Mungu anatakaje.
Nitoe wito kwa Wanawake woote Tanzania ya kwamba wafundisheni watoto maadili mema, hizi tabia za kuwapost tu watoto na kusema mziwanda wangu, kipenzi changu hazitoshi kuwafanya watoto wawe bora.
Kama kweli unampenda mwanao utamjenga na sio kumbomoa, leo hii tulalamika tuna viongozi mafisadi, je; unadhani ufisadi walizaliwa nao?
Naamini mmesikia na mtayatendea kazi , Asanteni