Ustawi wa Jamii: Tunajiandaa Vipi na Kuzuia Wimbi la Wazee Ombaomba wa Kesho ?

Ustawi wa Jamii: Tunajiandaa Vipi na Kuzuia Wimbi la Wazee Ombaomba wa Kesho ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Wahenga walisea Mchumia Juani Hulia Kivulini; Ila nadhani hawaku-consider kama cha kuchuma hakipo inakuwaje...;

Baba wa Taifa alisema katika Hotuba ya TANU (ambayo ndio Baba wa huyu CCM anayetawala Leo)

CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.
Kwa kukosa Ajira zenye Ujira tunazalisha watu wasio na Pensheni Hivyo Omba Omba wa Kesho
Vijana wa leo Wabangaizaji ambao mtaji wao ni nguvu zao na ni hand to mouth hawana kabisa akiba ya jioni let alone kesho au uzeeni wakiwa hawana mtaji wa nguvu. Makosa tunayofanya leo ndio yatakayoathiri Ustawi wa Kesho.

Mababu zetu Waliwezaje
Hapo kale watu waliishi sustainably mtu ana kashamba kake, kajumba kake na community inayomzunguka hivyo aliweza kupata Chakula (shambani) Malazi (Kajumba kake) na hata akiugua kuna dawa za kienyeji..., Pili mtu aliyejisomea alipomaliza aliweza kupata ajira zenye ujira wa kutosha wa kuweza kuwasomesha wadogo zake na kuwatunza wazazi wake; leo hii mzazi / mzee anauza shamba ili mtoto akasome na bado mtoto anarudi anakaa kijiweni au kuendelea kuomba hata pesa ya kunyolea ndevu..., hata akisema akabangaize kitaa anachopata hakimtoshi yeye let alone kutunza wazazi au kujiwekea akiba ya kesho yake.

Tutafanyaje ?
Hakuna Shortcut ya hili suala, bali ni kuhakikisha kunakuwepo Sera za kumuwezesha kila raia kuweza kuchumia juani ili aweze kulia kivulini (kula chakula na sio kulia machozi); kwa maana nyingine kila mtu awe na uwezo wa kupata ujira wa kutosha kutokana na ajira atakayofanya.

Bila hivyo tunaendelea kutengeneza Bomu la Hatari sana hapo kesho..., Ni aibu kubwa kwa Jamii kushindwa kuwaangalia wazee wake, na ni kosa pia kushindwa kutumia nguvu kazi hii iliyopo sasa..., huku kujidanganya kwamba kila mtu akawe mchuuzi wa bidhaa za watu huko ughaibuni is not sustainable....

Badala ya Kuwaangalia Viongozi Wastaafu na Wenza wao (Ambao wote Wanajiweza) Kwanini tusiangalie Wazee wetu;
Wawakilishi wetu kwa kutokujua kula na kipofu wamepitisha kabisa muswada wa kwamba hadi wenza wa viongozi wapate mafao..., Hii ni kama laana na kuwa out of touch sababu wakati hawa wanajiweza tayari na wameweza kujiwekea pensheni / mafao..., kuna huyu mzee ambaye hata pesa ya panadol hana kutokana na kwamba hakupewa ajira na mwisho wake uzeeni anakuwa ombaomba..., Je tuna wazee wangapi ? Hivi kweli tukisema kila mzee no matter what after 75 au 80 years of age apate hata laki moja moja kila mwezi pesa ya ugoro tutakuwa tumepunguza gharama za kununua Ma V8 Mangapi ?

Alijisemea Confucius
In a country well governed, poverty is something to be ashamed of, in a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.

Tusitengeneze Taifa la Chuki la Wasio nacho kwa Wenye Nacho......
 
miaka ya 2050 patakua na wazee wengi maskini Sadly wataishi terribly
Ni jukumu la Viongozi wa Sasa kuweka Sera na kuhakikisha hilo halitokei sasa hivi hakuna wazee wengi ombaomba sio bahati mbaya ni nguvu na busara iliyofanyika jana....

"Our future is created by what we do today, not tomorrow."
 
Vipi hakuna jibu ?; Ni nani atakayelaumiwa yule aliyetengeneza Tatizo (Sisi na Viongozi wa Sasa) au Yule atakayekumbwa na Tatizo ? Sababu kwa sasa naona kama tunajiliwaza hakuna Tatizo...
1729755622390.png
 
Back
Top Bottom