Ustawi wa Jamii wana wajibu gani katika kusimamia malezi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira Magumu?

Ustawi wa Jamii wana wajibu gani katika kusimamia malezi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira Magumu?

The mission 2017

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
1,748
Reaction score
3,229
Salamu wana bodi.

Kuna haja ya ustawi wa jamii kuongeza mikono yake kuwafikia watoto hasa walio na umri wa chini ya miaka 5, wanao ishi katika mazingira magumu.

Kuna wakati, Dunia inazunguka na kumuweka mtoto katika mazingira magumu sana, mpaka unajiuliza mtoto ameikosea nini hii dunia mpaka yamfike yote haya.

Tazama mifano ya aina hii ya watoto:

1. Walio zaliwa na akina mama vichaa, Kuna wanaume wajinga hua wanakamata vichaa na kuwatia mimba, baada ya miezi tisa unakuta kichaa yuko majalalani na mtoto mgongoni.

2. Walio zaliwa na akina mama homeless, hapa unaweza kuta mdada at age of 30/35 yuko chini ya daraja, kwenye kigodoro akiwa kakumbatia mtoto wa miaka 3.

Naongea hapa, nipo kituo cha daladala, pembeni yangu kuna binti 28 - 30 amejilaza chini na mtoto wa miaka 2. Mtoto analilia tu, na binti wa hajali.

Je, kama jamii hatuoni kua tunahaja ya kuweka fungu maalumu ustawi wa jamii, kwa case kama hii huyu mama ilitakiwa anyang'anywe huyu mtoto akalelewe sehemu nyingine au kama kuna wazazi wa kumu adopt waje kumu-adopt ustawi wa jamii.

Naomba kuwasilisha 💯
 
Back
Top Bottom