kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Wengi mnaofanya kazi za tiba,mtakubaliana nami kuwa Malaria imekuwa sugu kwa dawa zilizopendekezwa na wizara ya Afya Tanzania.Pamoja na ukweli huu kujulikana,hakuna tafiti za maana kuhusu tiba ya dawa nyingine inayoweza kutumika hapa nchini.Wasomi wetu wanasubiri Makampuni ya wazungu wakishirikiana na wahindi waje na pendekezo jipya kwa ajili ya majaribio ndipo utawaona jopo la wale wanaoitwa madaktari na wafamasia wakiwa channel ten asubuhi wakijidai kuelezea dawa hizo za majaribio kama kwanba walikuwepo wakati zinaandaliwa!Kwanini ninyi hamfanyi tafiti bali mnamwachia Ndodi na wenzake?Halafu baadae mnakuja kuwaponda akina Babu wa Loliondo!Hivi hili ni jukumu la nani kati yenu madaktari na wafamasia?Mmebaki kuuza dawa kwenye maduka yenu tu bila kujua kuwa sisi raia tunasumbuka sana na usugu wa malaria.Tuambieni mnafanya utafiti au tufanye wenyewe?
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums