Utaachwa kwenye mahusiano kwasababu ya uchafu

Utaachwa kwenye mahusiano kwasababu ya uchafu

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Shtuka! Usafi wa mwili wako ni jukumu lako....
Swaka kinywa chako zaidi ya mara moja kwa siku. Kama shughuli zako ni za juani baada ya kumaliza kazi koga vizuri na sugua vizuri kwapa zako, tena upake mafuta ya kukata harufu mbaya ya kwapa. Kwa wanawake mnaosuka, kama nywele za kichwani zimekushinda nyoa kuliko kuacha nywele zinatoa harufu mbaya - shtuka!.

1. Inawezekana kila siku unapoteza marafiki na watu wazuri kwasababu ya harufu mbaya ya mwili wako - shtuka!.

2. Unaweza kuachwa, kusalitiwa, au kuchokwa kwenye mahusiano kwasababu ya kunuka kinywa chako au kwapa.

3. Inawezekana ofisini unakwepwa na marafiki, kila unayetaka kuketi nae karibu anakukwepa. Kila mfanyakazi mwenzako unayemsogelea uzungumze nae kuhusu FILE anakukimbia au anatamani uondoke haraka kwa sababu ya harufu mbaya itokayo kwapani au kinywani mwako.

4. Huenda kila unapokutana na mwenza wako faragha hakupi raha za mdomoni kwa sababu unatoa harufu mbaya kinywani, na anaogopa kukwambia.

Shtuka! Mwenzetu ukiswaka leo asubuhi mpaka kesho asubuhi, siku nzima umekula miwali, mindizi, midagaa, maparachichi, maembe, chipsi na makolokolo mengine kibao halafu usiku huswaki kinywa chako unataka kumpa mdomo mwanandoa mwenzako.

Naam shtuka! Wapo watu ambao wakiwa wanazungumza na watu wanaonuka kinywa, nyuso zao huzielekeza pembeni ili kupisha harufu mbaya inayotoka kinywani mwa mzungumzaji. Si kila mtu unayezungumza nae akitazama pembeni anakuonea aibu, La hasha. Huenda unadhani mwanamke unayemtongoza hakutazami usoni kwasababu ya aibu kumbe anakwepa harufu mbaya unayotoa kinywani.

Shtuka! Usafi wa mwili ni jukumu lako. Usitegemee kwa umri wako atatokea mtu mzima mwenzako ambaye atakwambia unanuka kwapa au mdomo. Njia rahisi atakayochagua ni kukukwepa, kukuacha, kukuchukia, au kukuchoka kabisa - atatafuta mchepuko msafi na kila atakapoulizwa swali; Kwanini unamsaliti mwenzako? - atajibu; Aah! mambo ya ndoa ni mengi kweli kweli. Kumbe anatafuta furaha ya tendo, na furaha ya lile tendo ni usafi.

Shtuka! usafi wa mwili wako ni jukumu lako.

Right Marker
Dar es salaam.
 
Kweli...mtu ananuka kwapa mpk unajiuliza hivi ana mpenzi kweli....
 
Back
Top Bottom