Utaalamu unavyotumika vibaya kuidanganya Serikali

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Katika jina la JMT kazi iendelee,

Kichwa cha andiko hili kisihusishwe kabisa na kupinga mawazo ya wataalamu au kupinga utaalamu unaofanywa na wataalamu mbalimbali katika kuishauri Serikaki juu ya miradi na masuala mbalimbali.

Wataalamu wamekuwa wakitoa mchango mzuri lakini wapo waliokuwa wakitia kwa kuangalia zaidi maslahi yao binafsi na siyo ya Taifa, hawa ndiyo wanaobeba kichwa cha andiko hili.

Tarehe 24/4/2021 Mbunge wa Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji akiwa katika Ziara yake Wilayani Mbogwe alisema upo mradi wa kutoa maji katika Ziwa Victoria uliokadiriwa kugharimu shilingi bilioni hamsini na mbili lakini mradi huo kwa sasa unatekelezwa kwa shilingi bilioni nne.

Hiyo ni Wizara moja tu ya maji, unaweza ukajaribu kutafakari na kuona kama Wizara nyingine wanafanya hivyo hivyo hali ipo vipi? Majibu ya Serikali mara kadhaa yamekuwa yakipingana na hali halisi ilivyo. Mathalani, tarehe 14/4/2021 Naibu Waziri wa maji alisema hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Wilaya ya Mbogwe ni asilimia 55% jambo ambalo hata Mbunge mwenyewe alilishangaa na kukataa bungeni.

Hali hii inaonesha huenda watendaji wa chini wanadanganywa hawaendi kwenye uwanja wao wa kazi kuona au wanafahamu uwanja wo ulivyo na wanaamua kwa makusudi kutoa taarifa na takwimu za uongo ili kulinda nafasi zao kwa maslahi yao na siyo maslahi mapana ya jamii.

Ushauri wangu juu ya hali hii ni Serikali ikubali gharama ya ufuatiliaji na uwajibikaji. Hapa namaanisha taarifa yoyote ya Serikali kabla haijafikishwa kwa Umma ni vizuri viongozi wenye dhamana wakajiridhisha kwa kufuatilia ili kuiepushia Serikali kutoa majibu ya uongo katika masuala mbalimbali jambo linaloitia doa na aibu.
 
Ukizingatia hao uliowataja ni wateule wa mtu aliyeiongoza Tz kwa msingi ya uongo, basi ni mpaka hao waliochaguliwa kwa njia za uongo watakapoondoka, ndio ukweli utakapotamalaki. Tumedanganywa vya kutosha!
 
Katika jina la JMT kazi iendelee,
Kichwa cha andiko hili kisihusishwe kabisa na kupinga mawazo ya wataalamu au kupinga utaalamu unaofanywa na wataalamu mbalimbali katika kuishauri Serikaki juu ya miradi na masuala mbalimbali.

Wataalamu wamekuwa wakitoa mchango mzuri lakini wapo waliokuwa wakitia kwa kuangalia zaidi maslahi yao binafsi na siyo ya Taifa, hawa ndiyo wanaobeba kichwa cha andiko hili.

Tarehe 24/4/2021 Mbunge wa Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji akiwa katika Ziara yake Wilayani Mbogwe alisema upo mradi wa kutoa maji katika Ziwa Victoria uliokadiriwa kugharimu shilingi bilioni hamsini na mbili lakini mradi huo kwa sasa unatekelezwa kwa shilingi bilioni nne.

Hiyo ni Wizara moja tu ya maji, unaweza ukajaribu kutafakari na kuona kama Wizara nyingine wanafanya hivyo hivyo hali ipo vipi? Majibu ya Serikali mara kadhaa yamekuwa yakipingana na hali halisi ilivyo. Mathalani, tarehe 14/4/2021 Naibu Waziri wa maji alisema hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Wilaya ya Mbogwe ni asilimia 55% jambo ambalo hata Mbunge mwenyewe alilishangaa na kukataa bungeni.

Hali hii inaonesha huenda watendaji wa chini wanadanganywa hawaendi kwenye uwanja wao wa kazi kuona au wanafahamu uwanja wo ulivyo na wanaamua kwa makusudi kutoa taarifa na takwimu za uongo ili kulinda nafasi zao kwa maslahi yao na siyo maslahi mapana ya jamii.

Ushauri wangu juu ya hali hii ni Serikali ikubali gharama ya ufuatiliaji na uwajibikaji. Hapa namaanisha taarifa yoyote ya Serikali kabla haijafikishwa kwa Umma ni vizuri viongozi wenye dhamana wakajiridhisha kwa kufuatilia ili kuiepushia Serikali kutoa majibu ya uongo katika masuala mbalimbali jambo linaloitia doa na aibu.
Ukitoka mbongwe unakwenda bukombe jimbo la doto Biteko waziri wa madini. Kwà mantiki hiyo ni aibu hadi leo hakuna maji bukombe na mbongwe
 
Dah....nimekumbuka DARAJA letu la Jangwani litakalo inuliwa kwa mita 300 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom