Utabiri: Huenda ya KANU nchini Kenya yakaikumba CCM

Hahahaha Labda uwadanganye kama vita vya maji maji ndo utawakamata wengi sanaaaa
 
Mimi kinachonishangaza ni The so called the State kukalia kimya uovu wanaofanyiwa watanzania wa vyama vingine na serikali ya ccm!!!Hadi najiulizaga mimi kweli Hawa jamaa ni wanaccm au watanzania wenye mapenzi mema na hii nchi kweli?? CCM ilipaswa kuondolewa mapema Sana tangu 2010 coz imeua watu Sana ili kulinda maslahi ya wachache!!!!Inawezekanaje mtu anachinjwa vile kama nyama buchani Alphonsi mawazo?? inakuaje tena kwenye nchi inayoitwa ni kisiwa cha amani??? THE State popote mlipo naomba mjiuzulu hampo kwao ajili ya Taifa mnalinda ujambazi na wizi na magenge ya uhalifu yanayohatarisha amani ya nchi yaitwayo serikali ya CCM!!!!kama mpo humu msome na mfahamu!!!Mimi mwenye ndoto ya kuwa Raisi wa nchi hii kwa kupitia chama cha umoja party Nitaondoa upumbavu wa chama cha siasa kumiliki Mali za umma na kuziita zao Mali zote ziwe za serikali na za watanzania wote sio za chama wala za mtu binafsi!!!ujinga wa ruzuku za vyama za siasa ndio chanzo cha mauaji ya watu hivyo!!!mishahara ya wanasiasa itashushwa na watumishi wa umma kuongezewa wao ndio wanaowatumikia wananchi!!!nitaifanya siasa usiwe tena kimbilio la wenye uchu wa mapesa mengi bali wazalendo wa kweli!!na Mengi nitafanya ili utanzania uwe wa kujivunia na sio Kujivunia wanasiasa na majina yao!!!vyama vitakuwa taasisi za kawaida tu sio mapesa na ufisadi wa kutisha kama tunavoona!!siasa ndio inaharibu nchi hasa chama tawala!!!hakutakuwa na chama kitakachoshika hatamu kwa miaka zaidi ya mitano ili kuonyesha nchi sio ya chama kimoja!!!chama kujaa madarakani kwa muda mrefu huleta Mungu watu na ufisadi kutamalaki!!hiyo sitoruhusu!!!Nitaifumua Deep State na nitawauliza mlikuwa wapi wakati ccm na serikali yao inaua watu hovyo kisa itikadi za uchama nitawaambia nyie ndio chachu ya matatizo ya nchi yetu na ufisadi uliotamalaki hadi sasa!!!
 
Sina lakusema ila kuepusha hili kunankitu kitafanyika... Soma vozuri uzi wangu.. nimeeleza japo sijafunguka vile ukanielewa.
 
Unabii wa baba wa taifa karibu kutimia...Tuombe tu iwe kwa amani na tusiumizane kama wao hao Kenya
 
Kama kutakuwa na umakini katika kuwa pick wale ambao wana clean hands kwa pande zote mbili bila kujali u vyama na kutengenez transition nzuri wala hii hofu haipo kabisa...Tatizo ni ku mix wenye uovu na wenye moral conscious na kusababisha dilemma ya ajabu kwa taifa...Salama yetu ni kukubali haki kutoa mwafaka wa kitaifa...

Kama nabii nasema hivi naujua mwisho kabla ya mwanzo...2012 was a determinant year we are very close to the end which is the new beggining of new era...Mwanzo ambao Tanzania itakuwa nchi ya kupigiwa mfano duniani...Ila lile giza lile nililoliona ndilo ambalo kila siku naomba Mungu aliondoshe!
 
Sina lakusema ila kuepusha hili kunankitu kitafanyika... Soma vozuri uzi wangu.. nimeeleza japo sijafunguka vile ukanielewa.
Achaa kama ni kitu
Chema kitokee
Tanzania
 
Reactions: Ame
Huko tuendako uwenda chama kitakuwa na wakati mgumu sana kutokana na madhila na matukio watanzania wameona chini ya CCM.

Nina tia shaka wakuu wa Taifa hili ipo siku watasema bora kuvunja chama kuliko kubaki wamoja wakati ktk mioyo hatupo wamoja.
 
Sasa hivi wanamuimba Samia. Mara Samia katoa hela hii, mara Samia katoa hela ile, yaani wanaendelea kuimba pale wapambe wa Magu walipoishia. Aisee, sijui huyo Samia ni tajiri kiasi gani? Ukipita Ubungo flyover kwenye yale manguzo ya mataa utaona mapicha yake unaweza ukadhani uko Cairo Egypt enzi za Hosni Mubarak.
 
Ngoja waje Buku 7 wa UVCCM wakushambulie hadi ukimbie humu, wenzako CCM ndo mungu wao halafu uwaambie eti itakufa,wanaona unatania tu
 
huo sio utabiri; ukishasema huenda, neno huenda lishaharibu maana halisi ya utabiri unakuwa kama unabahatisha. Nenda direct.

Afu utabiri wako wa leo ni wa kitoto, hata mtoto mdogo anajua ipo siku ccm itavunjika tuu
 
Wakati wa KANU mpaka Chifu alikuwa na nguvu kuliko Mkuu wa Jeshi yaan akiitana mkutano alafu ugome kufika utajuta.
 
Kitakaa miaka 100 kwa maana kinamiliki jeshi la polis na Tume ya kupiga kura.
Suala la kupiga kura haliwezi kuking'oa.Ona 2020 kimeshinda wabunge kwa asilimia 99.999999%
 
Huu utabiri unatimia 2025 baada ya wana ccm nao kuchoka, liwalo na liwe. Hatuwezi kuongozwa na Samia
 
Ooh! rais asiguswe akiguswa nchi itatikisika nchi itayumba, swali mbona amekufa na tumebaki salama? hayo maneno yenu ni uzushi tu ili mlinde maslahi yenu.
 
Ili jambo hili litokee Tanzania state machineries lazima watambue kuwa Tanzania ni kubwa na muhimu kuliko CCM kama Kenya walivyotambua kuwa Kenya ni kubwa kuliko KANU na Daniel T. Arap Moi.

State machineries wanajua chama X au Y kiwepo madarakani hawatakiwi kuwa na personal but maslahi yao ni Tanzania salama.

State machineries zinafamu wazalendo wapo kwenye vyama vyote vya siasa na wahuni vivyo hivyo wapo ni suala la muda mambo yatakuwa safi kabisa.

Ukombozi wa kwanza ulishapatikana Uhuru wapili vyama vingi vya siasa na watatu ambao ni katiba mpya upo njiani unakuja siyo lazima upiganiwe kwa nguvu kila mtu anajua umuhimu wa katiba mpya. CCM wenyewe wanalifahamu hilo ni suala la muda katiba mpya yuko safarini anakuja Tanzania kikubwa tuwe wazalendo ni suala la muda tu utafika muda siyo mrefu.

Huyu katiba mpya ni mgeni ambaye kila mmoja wetu atamfurahia atatufundisha haki sawa atatufundisha demokrasia atatufundisha uhuru wa mihili ya serikali atatufundisha ushirikishwaji atatusaidia kupambana na viongozi legelege bila uonevu wa aina yeyote lakini kupitia haki. Huyu mgeni tusikate tamaa amesha abiri ndege anakuja Tanzania.

Akifika tumpokee wote na kumsikiliza na kufuata maelekezo yake na Tanzania itapaa kwa kasi.
 
Hapo ni unaonyesha unafiki na roho ya ajabu ya kiafrika.

Mwanafunzi kupewa maziwa haikuwa hisani ya Moi au mkuu wa nchi ni utaratibu ulikuwepo kwa nchi za kiafrika tatizo ni utekelezaji ndiyo shida hata ulipaji wa ada kwa shule za msingi na secondary vile haujui nchi huwa zina malengo gani na wanapokuja wanasiasa ndipo mnaambiwa ujinga.

Issue ya somo la history, nani kakwambia jiwe ndiye lilikuwa lengo, unafiki huo?.

Kuvaa beji ya Moi hakuna mwanafunzi alilazimishwa kipindi hicho labda kama ulisimuliwa, mfano toka kipindi cha JK beji zilianza kusambaa na watu kuuza hata sasa zipo za BiM mbona tunapewa au tunanunua na tunavaa!.

Nitakuwa napingana na watu kama wewe kwa sababu ya roho mbaya, fitina, ufitinishi wenu wa kiafrika kwa sababu za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…