Hata warumi hawakuwahi kufikiri utawala wao utafikia mwisho pamoja na kutawala dunia kwa miaka mia tano. Mabadiliko huwezi kuyaona kila wakati, yanaweza kutokea ghafla.
Siyo vifo vyote hutokea mpaka uugue kwanza No. CCM imevuruga maisha ya watu wengi sana.
CCM aliyoianzisha Nyerere, hata yeye mwenyewe angekuwa hai, angeikataa na pengine kujuta kwa kile alichokianzisha kuwa chombo cha mateso kwa watu wake.
Tuliyoyashuhudia wakati wa Magufuli, CCM waliona na walinyamaza kimya . Hii kumfunga Sabaya na kutaka kumkamata Makonda wamesubiri mpaka Magufuli amekufa, Magufuli kuwa mwenyekiti hakuwezi kuwa sababu ya CCM kunyamazia uovu,ndio maana wanna vikao vya ngazi mbalimbali. Mahakama zimemkamata na hatia Musiba kipindi hiki.
CCM ya Nyerere pamoja na mapungufu yake iliheshimu Sana uhuru wa mahakama. Mwalimu alikuwa na mapungufu Kama mwanadamu na alikiri upungufu wake, lakini kwenye chombo Cha utoaji haki hakuingilia kabisa hata hotuba yake alipokumbushia Vita ya rushwa kipindi Chao na ikatokea waziri wake Fundikira akapatikana na makosa ya rushwa alipelekwa mahakamani lakini kwa kuwa mahakama ilikuwa huru haikuamua kufuata Utashi wa kisiasa Kama ilivyo leo na tunamuona Jaji mkuu anahudhuria kwenye mialiko ambayo ajenda zake zitakwenda mahakamani au ziko mahakamani na yeye bila haya anachangia. Upo wapi Uhuru wa mahakama chini ya CCM ya leo!!!
CCM imara isingeruhusu hayo. CCM ilinyamaza kimya hata pale kulipokuwa na tetesi za kuongezewa muda Magufuli kinyume Cha katiba.
Salmin Amour Rais wa Zanzibar wakati wake alijaribu kutaka kujiongezea muda CCM iliyokuwa imara wakati huo hawakumuogopa.
Leo CCM uongozi wanapeana wao wanaojiita wenye CCM na watoto wao. CCM imara isingekubali kuvunjwa kwa katiba kwa kuzuia vyama vya upinzani kufanya mikutano. CCM ya Sasa ni waoga usipime. Hawana watu wa kuaminika tena. Watu waliawaamini wanasiasa wasomi enzi hizo, siyo Sasa. Nani angeaacha kufuatilia majadiliano kwenye Meza ya duara kutoka redio ya ujerumani kama ukisikia leo atakuwepo, Prof Haroub Othman au Prof. Chachage au Mzee Kigunge!! Lakini kipindi tumewaona kina Kitila,Kabudi, Bashiru wote ni mashahidi,mambo mengi yameharibika wakishuhudia na wako kimya. Mbunge anapigwa risasi mchana kweupe na mwisho anavuliwa ubunge wake hawa wako bungeni wanashangilia.
Wachache waliobaki CCM hawapewi heshima kwa sababu wanapenda kusema ukweli. Mzee Warioba,Butiku na hata Jenerali ulimwengu wanapuuzwa.
Hivyo anguko la CCM halitashangaza kwani tayari ilishaanguka kwenye mioyo ya watanzania wengi imebakiza nguvu za dola tu.