UTABIRI: Muda si mrefu hapatashikika hapo Yanga SC

Mac Alpho

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
13,953
Reaction score
27,825
Mechi za marudiano ya michuano ya CAFCL na CAFCC ni week ijayo tu ambapo Simba SC na Yanga kwa pamoja zitazitupa karata zao za mwisho kuwania nafasi za kuingia hatua ya makundi, katika hiyo michezo Simba SC kwa kiasi fulani wanayo matumaini huku Yanga SC ikionekana kuwa na mlima mrefu sana.

Fikiria Yanga iende Sudan ikapokee kipigo kizito kutoka kwa Al Hilal itoke kwenye michuano ya CAFCL, kisha wiki moja baadae ikutane na Simba Sc iliyotinga hatua ya makundi ifungwe na kupoteze huo mchezo. Amini nawaambieni kutatokea mvurugano mkubwa ambao hamjawahi kuushudia kwenye hiyo club, yani hapatakalika kabisa.

Mtasikia mengi sana ikiwa ni pamoja na kutaka professa wao afutwe kazi (hasa wakitolewa hata hilo shirikisho), watakumbuka na kulaumu ya Hersi kupita bila kupingwa, usajili Aziz Ki, Kambole, Lomalisa, Bigirimana utajadiliwa upya na kuonekana ni wa kijinga ingawa kwasasa hawataki kukubali kuwa walipuyanga n.k.

NB: Hayo niliyoeleza hapo juu nayaona yakienda kutokea, vuteni viti mkae mkao wa kusubiria.
 
Mimi kwenye maisha yangu nimekutan a na mambo ambayo yashakufa kabisa ,ukingalia unasema sitoboi .Mashabiki Siyo Mungu lolote linaweza tokea .
 
Wafurukute waanzie makundi ya Shirikisho ndio level yao, sio kukimbilia makundi ya kaka zao wakati bado wananukia maziwa.
 
Mechi za marudiano ya michuano ya CAFCL na CAFCC ni week ijayo tu ambapo Simba SC na Yanga kwa pamoja zitazitupa karata zao za mwisho kuwania nafasi za kuingia hatua ya makundi, katika hiyo michezo Simba SC kwa kiasi fulani wanayo matumaini huku Yanga SC ikionekana kuwa na mlima mrefu sana.

Fikiria Yanga iende Sudan ikapokee kipigo kizito kutoka kwa Al Hilal itoke kwenye michuano ya CAFCL, kisha wiki moja baadae ikutane na Simba Sc iliyotinga hatua ya makundi ifungwe na kupoteze huo mchezo. Amini nawaambieni kutatokea mvurugano mkubwa ambao hamjawahi kuushudia kwenye hiyo club, yani hapatakalika kabisa.

Mtasikia mengi sana ikiwa ni pamoja na kutaka professa wao afutwe kazi (hasa wakitolewa hata hilo shirikisho), watakumbuka na kulaumu ya Hersi kupita bila kupingwa, usajili Aziz Ki, Kambole, Lomalisa, Bigirimana utajadiliwa upya na kuonekana ni wa kijinga ingawa kwasasa hawataki kukubali kuwa walipuyanga n.k.

NB: Hayo niliyoeleza hapo juu nayaona yakienda kutokea, vuteni viti mkae mkao wa kusubiria.
sipingi utabiri wako lakini ulichotabiri hakina asilimia yoyote kutokea meza itapinduka kulia kushoto..... niko pale nimekaa
 
Back
Top Bottom