UTABIRI: Simba SC 1 -3 Yanga SC Kariakoo Derby, Novemba 5, 2023

DINHO

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
880
Reaction score
1,750
Imenichukua mwezi mmoja kufanya analysis juu ya hii game, nimeangalia game karibu 10 za kila timu na katika hizo karibu game 5 nilienda uwanjani kushuhudia tactics za timu zote mbili.

Game ya 05/11 ni moja ya game ngumu kwa mwonekano wa nje, ila kwa namna nilivyoziangalia hizo timu zote, 75% Yanga ataibuka na ushindi wa si chini ya Magoli 4 kwanini nasema hivi shuka chini;

1. UKUTA/MABEKI
Timu zote mbili msimu huu ziliimarisha safu yake ya ulinzi, lkn safu ya Yanga iko imara zaidi, kwani katika game za 11 alizocheza za kimashindano ameruhusu magoli 5 tu, wakati Simba imeruhusu magoli 11.

Udhaifu wao
YANGA udhaifu mkubwa upo kati hasa akicheza MWAMNYETO na hapa Simba wakimtumia vizuri NTIBAZANKIZA wanaweza kupata bao au hata Penati. Pia upande wa kushoto LOMALISA sio mtu kazi ni mtu Smart hivyo akipata mtu kazi kama KIBU game itakuwa ngumu mno wa upande huo wa kushoto.

SIMBA hawa wana udhaifu mkubwa zaidi katika safu yao ya beki, uwe Pembeni au kati, pande zote zinapitika kirahisi na hasa ikitokea wao wametangulia kufunga. KAPOMBE, ZIMBWE wamechoka tayari kutokana na kutumika kwa muda mrefu, CHEMALONE na INONGA wanacheza show game ambazo zinahatarisha sana ulinzi wao. Mf. Game na Al Ahly kama sio uzembe wa washambuliaji wa Al Alhy basi Simba walipaswa kufungwa si chini ya magoli 5.

USHAMBULIAJI
YANGA wanaonekana wana safu nzuri zaidi ya Ushambuliaji ukilinganisha na Simba kwana hadi game 11 za mashindano walizocheza tayari wamefunga magoli 30. Wakati wenzao SIMBA wako na magoli 22 katika game 10.

Angalizo:
Simba wanatakiwa kucheza kwa mfumo wa Counter attack ili kuwamudu Yanga, na tofauti na hapo kilio kitakuwa kizito kwa SIMBA.

Yanga wanatakiwa kuangalia safu ya beki kama kuna uwezekano waanze JOB na BACCA ili kupunguza risk za faulo ambazo hazina maana.

NB: Uchawi upo na unafanya kazi, ila kwa uhalisia wa vikosi na kwa jinsi wanavyocheza natabiri matokeo kuwa SIMBA 1-3 YANGA
 
Kwa uchambuzi wangu

Kabla ya mechi kuanza tayari Simba kasharuhusu goli Moja Kwasababu ya poor defense ya Simba kuruhusu goli Kila mechi msimu huu... tofauti na defense ya Yanga ambayo Ina ukuta imara sana ( ukuta wa yericko).....ukiachilia mbali magoli machache walioruhusu ..... even machine doesn't work 100% efficiently

Hivyo basi mpaka Sasa Yanga wanaongoza goli Moja ......dhidi ya kolos...
 
Ndio maana kule mkwakwani simba alikufa goli kwa yanga ndani ya kipindi cha kwanza kweli ukiwa utopolo akili zinahama kabisa.
 
Endelea kutabiri Mkuu

Wenye akili wanasubiri tarehe ya mchezo husika na Dakika zake 90.

Muda ni hakimu mwema utatoa majibu.
 
Yeyote humu anaepiga ramli Yanga itashinda utakuta ana mahaba na Utopolo.

Anaeitabiria Simba utakuta ana mahaba na Simba.

Tabiri hizi utaona Ni km hazina maana yyte zaidi ya umaandazi.

Derby ya Kariakoo siyo rahisi km unaichambua Geita vs Yanga.

Hakuna anaejiamini kwamba atamfunga mwingine. Maandalizi ya ndani na nje ya uwanja ndiyo huamua hii mechi. Anaestahili na kutengeneza anaweza asishinde.

Nb: Hakuna Simba Wala Yanga mbovu hizi timu zinapokutana.. Ni mechi yenye Mambo mengi mno.Inawezekana hii mechi tayari ilishachezwa.

Umdhaniaye ndiye siye!
 
Makolokolo SC fans ni pumba tupu, ukiyakosoa tu tayari yamenuna na matusi juu, yani yawe yanasifiwa kila siku kama Watoto wadogo wanaobembelezwa kulala [emoji848]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Msisahau Robertinho ni master anaweza akaicheza mechi kwa namna mbili au Tatu tofauti,

1.akicheza kwa high pressing yanga anakufa kwa Aina ya beki zake na kiungo wake hususani Aucho ambae ni Holding.Aucho hapendi mgongane au mkae karibu karibu maana yeye ndio anapoza timu na anaamua timu ichezeje akipokea past kutoka kwa beki zake za Kati au moja kwa moja kwa Diarra ukifanya pressing eneo hili ambao yanga ni hatari sana katika kuanzisha mashambulizi utafanya timu igawanyike iliokua Chini na iliokua juu.yanga hivi karibuni wanacheza 4-2-3-1 Max ndio mtu hatari kushuka chini na kupandisha mipira juu kupitia katikati au pembeni ukiblock hili eneo unaweza kuwafanya wasiwe hatari

2.Simba tukacheza kama na AL ahly misri au na Yanga mechi ya Ngao tunawaachia mpira wacheze tuwashambulie kwa kusitukiza kupitia pembeni kwa Limalisa au Yao Yao wanapokua wamepanda na kuwapigia mipira mirefu. Pia kuwa hatari kwenye set pieces maana tunaonekana kuwa ni eneo imara kwetu siku hizi na ndio eneo dhaifu la Yanga kufungwa.
 
Hahaha! Utopolo kweli vilaza, hivi tushindwe kuwafunga kwa timu gani. Mnadhani kirahisi tu mtazuia mashambulizi ya Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…