Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UTABIRI WA AL HABIB SAYYID OMAR BIN SUMEIT
Al Habib Sayyid Omar bin Sumeit alitabiri kuwa Zanzibar itarejea katika hali yake.
Alisema maneno haya ya kutia matumaini baada ya kushuhudia mapinduzi na yaliyofuata baada ya Mapinduzi.
Katika kitabu kipya "Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama Kutoka Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam," nimeandika habari za Al Habib Sayyid Omar bin Sumeit.
Miaka ya mwanzoni 1940s Al Habib alikwenda Machame sehemu inayoitwa Kalali kufungua Msikiti wa kwanza wa Ijumaa Uchaggani na alipokelewa na Chief Abdiel Shangali aliyeapa baada ya kuchukua utawala kutoka kwa Baba yake kuwa hataruhusu Uislam kuingia katika nchi yake.
Rajabu Ibrahim Kirama kwa juhudi kubwa aliweza kuuingiza Uislam Machame Nkuu kwa msaada Sheikh Hassan bin Ameir mwanafunzi wa Sayyid Ahmad bin Sumeit baba yake Al Habib.
Miaka ya mwanzoni 1940s kama inavyoonyesha hapo juu Sayyid Omar bin Sumeit alifika Kalali kijiji si mbali na Nkuu kufungua kwa takbir msikiti wa kwanza wa Ijumaa Uchaggani.
Leo nyaraka za historia hii zimehifadhiwa na ukoo wa Mzee Rajabu kwa takriban miaka 90 hadi zimetufikia kwa rehema zake Allah na Allah katuwezesha kuandika kitabu cha historia ya Uislam Uchaggani historia ambayo ilikuwa imepotea.
Sheikh Hassan bin Ameir alipokwenda Machame 1945 alimshukuru Chief Shangali kwa ukarimu wake kwa mapokezi ya Mufti wa Zanzibar Sayyid Omar bin Sumeit.
Tukitazama nyuma katika mienendo ya mabwana hawa wakubwa na maneno yao hapana shaka faraja itarejea.
Nani katika sisi aliyajua haya ya Al Habib, Chief Shangali na Msikiti wa Ijumaa wa Kalali Machame?
Nani aliyejua kuwa katika nyumba ya mtoto wa Rajabu Ibrahim Kirama, Salim Rajabu darini kwake katika magunia kuna nyaraka zilizohifadhi majina ya mabwana wakubwa hawa waliotoka Zanzibar hadi Kilimanjaro Uchaggani kuwaita ndugu zao kati salama na amani?
In Shaa Allah Zanzibar itavuka mitihani hii yake ya damu na machozi kama alivyotabiri Al Habib Sayyid Omar bin Sumeit.
Amin.