Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein watimia

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,191
Reaction score
677
Sheikh Yahya Hussein alitabiri kuwa mtu yeyote ataeshindana na Kikwete atakufa. watu wengi walikanusha na kumbeza, wengine walidiriki kusema mzee amechoka na hana mpya.


kumbe utabiri wake una ukweli wa kutosha, wengi tulifikiri kufa ni kutoka roho tu. lakini hata kufa kisiasa ni kufa



kwa hio ndugu yetu shibuda aliepambana na Kikwete tayari ameshakufa kisiasa
 
Wewe acha maneno yako, Yeye alimaanisha kuondolewa uhai, na kuondoka CCm siyo kufa kisiasa. Ivi wewe una maana kuwa hai ni kuwa sisiemu? Ndugu yangu kama utakuwa hivyo basi hii nchi haiendi mbele hata kidogo. Kwa sababu tunaona kwenye vyama vingine pia kuna kitu kinaendelea si wote wamekufa.

Please re think.
Huu ni mwelekeo wa kufa kwa CCm na siyo watu wanaohama. CCM uhai wake unazidi kuzeeka!!!
 

Mzee wewe wajua hii ni PUMBA!
Kwani wewe msemaji wa Sh Yahya, au mko dili moja huko kusadikika?
 
Mzee wewe wajua hii ni PUMBA!
Kwani wewe msemaji wa Sh Yahya, au mko dili moja huko kusadikika?

Kweli hii ni pumba LIVE bila chenga.

Na nadhani huyu ni mwenzie au shabiki wake
Maana kuhama si sawa na kufa
 


POle saana kwa kuoza akili Mungu akurudishie akili zako
 

Yaani ndugu yangu unavyobadilisha kauli utadhani Watanzania hatuna masikio!!
Ndo maana swahiba wako (Shekh Yahya) amepunguzwa makali na Pweza Paul.
 

Nani kakwambia Shibuda kafa kisiasa?Nyie ndio wale msiopenda mabadiliko katika jamii.
Msalimie baba yako Shehe Yahaya natumai ujumbe aliokutuma umefika hata kama ni pumba tupu.
Natumai pia kakutabiria kuwa umefilisika kifikra na pole pole utakufa na hatutokuona tena humu kutuletea pumba kama hizi.

 
[QUOTE said:
sheikh yahya hussein alitabiri kuwa mtu yeyote ataeshindana na kikwete atakufa. watu wengi walikanusha na kumbeza, wengine walidiriki kusema mzee amechoka na hana mpya....








  1. sikubaliani nawe kwani unajaribu kulazimisha watanzania tuamini katika nguvu za majini (imani yako) na bila shaka alipopondewa ulikaa kimya na sasa sononeko lako limekwisha lakini nakwambia huo ni uchovu wa mawazo kwani umeungaunga tu matukio ukidai ni picture in continuum.
  2. naona uko mbali kweli na dunia. hakuna mwana ccm yeyote aliyeshindana na kikwete; kura zilipigwa au kwa kikwete (ndiyo) au kwa ruhani (hapana) ambapo ruhani alipata kura 16 tu za wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa ccm na zilizobaki akanyakua jk
 
Mzee wewe wajua hii ni PUMBA!
Kwani wewe msemaji wa Sh Yahya, au mko dili moja huko kusadikika?
.

Wakuu,
Mbona mnashambulia sana mleta maada?Hayo ni maoni yake tu.
Kumbuka uchaguzi wa mwaka 2005,Sheikh Yahya,alitabiri kuwa mshindi katika ushaguzi huo angekuwa mwanamke.Na baada ya JK kushinda, Yahya ,alisema alikuwa na maana ya mshindi mwenye mvuto wa mwanamke.

Kwa hiyo inawezekana mleta maada akawa yuko sahihi.
 
Aliyekuroga wewe alikufa mwaka jana! Ondoka hapa na upuuzi wako!
 
Shibuda alipambana na Kikwete LINI?
 
wewe ni nani mpaka uongee kwa niaba ya shk yahya..?

kwani yeye hajui tofauti kati ya kufa na kufa kisiasa..?
 
CCM na vibaraka wao matumbo joto.Mara wajaribu kete ya udini,mara wageukie ushirikina.Mshindwe na mlegee kabisa mafisadi wakubwa nyie.
 
Kwani SHe Yahaya ni nani bwana, nyie mnapeeendaa kuwausudu watu wasio na Fasida katika Taifa,, ok Baada ya utabiri huo wewe umepata nini, na kikwete si Mtu kama wewe ulivyo, sasa Toka 2000 mbona ameshindana na wengi tu hawajafa,, Lipumba, Mrema, Mtikila, Mbatia hawa hujawahi kuona wala kusikia, au mashindano unayosema wewe ya Nusu marathon?

Hebu jaribu kufikiri na kutenda kabla ya kuja Jamiini...
 

mtoa mada kushambuliwa ni halali yake. Maana hili si jukwaa la propaganda na ubabaishaji kama wanavyotaka kulitumia yeye na huyo mzee wake. Hapa ni mahala pa fikra pevu na mtazamo chanya. Kama wanataka jukwaa la upotoshaji waungane na wapotoshaji wengine akina tambwe hiza na kingunge waanzishe lao. Ukiona hivyo wanatengeneza mazingira ya kuleta uongo mwingine.
 
Shibuda hakufa kisiasa bali alijambaziwa kura za maoni kama sera za chama cha majambazi, akija CHADEMA atapaa sana kisiasa kwani CHADEMA ni chama cha demokrasia na makini sana hakiibi.Sheikh Yahaya lazima amlinde JK kwani ndie aliyemsaidia kwenda india kwa matibabu, so lazima atishie watu ili wasimpinge lakini hakuna kitu hapo.
 
kazi kweli kweli kufa nini kwani?nisaidieni na mimi jamani
 
na bahati mbaya sana leo kusaini tu kwenye JF nakutana na pumba za Mtu Pwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…