Wapendwa wana JF, ni matumaini yangu mko vizuri.
Nimeota mara kadhaa kwamba Wakili Msomi Mwabukusi atakuja kuwa kiongozi mkubwa kabisa katika nchi yetu.
Atakuwa ni Rais mpole na mnyenyekevu kuliko wote waliomtangulia. Lakini wakati huo huo, atakuwa ni Rais mkali zaidi kuwahi kutokea Tanganyika.
Wakati wa utawala wake, kutakuwa na ustawi wa watu na vitu. Raslimali za Taifa zitatumika kuwanufaisha wananchi wote bila upendeleo.
Nimeota, tena nimeoneshwa kwamba wahitimu wengi wa vyuo na vyuo vikuu ambao wamejazana mtaani, wote watapata ajira serikalini bila kujalisha umri wao wala miaka waliyohitimu. Na kwa wale ambao hawataajiriwa kwa namna moja ama nyingine, nimeoneshwa watakuwa wanalipwa posho kila mwezi!
Nimeoneshwa Watanganyika wengi wakimiliki nyumba na magari mazuri kwa gharama nafuu zilizochangiwa kwa kiasi na serikali yao.
Nimeoneshwa huduma za Afya na Elimu zikitolewa bure kwa kila mtoto wa Kitanganyika.
Nimeoneshwa pia hakutakuwa na katika katika ya umeme kwa kipindi chote atakachokuwa kiongozi.
Nimeona Watanganyika wengi wakimwongezea muda wa kuongoza kutokana na upendo, uadilifu, upole na unyenyekevu wake katika kuwaongoza Watanganyika.
Nimeona mabadiliko ya Katiba bora kabisa kuwahi kutokea Afrika, katiba ya mfano yakifanyika katika Katiba ya Tanganyika.
Nimeona mafisadi wakifunguliwa kesi, kufungwa kifungo cha maisha na wengine kunyongwa hadi kufa.
Tena nimeoneshwa fedha ambazo mafisadi hao walizoliibia Taifa kwa namna moja ama nyingine, zikitaifishwa na kuwanufaisha Watanganyika wote.
Kwa ufupi, nimeota na kuoneshwa Tanganyika inayomeremeta na kustawi huku ikiongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika chini ya utawala wa Mh. Wakili Msomi Boniface Mwabukusi.
Mungu ibariki Tanganyika,
Mungu mbariki Mwabukusi,
Amin.