UTABIRI: yatayozungumzwa na JPM kesho tar 1May 2019 siku ya Wafanyakazi

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Kesho ni siku ya wafanyakazi Duniani na mgeni rasmi ni ráis JPM mkoani mbeya,tutabiri yatayozungumzwa .
--Uhakiki umebaki na ukimalizika ataongeza mshahara kweli kweli tumpe muda.
--Mishahara hewa bado ipo na anapambana nayo ili akiongeza aongeze pakubwa.
- Tume ya mishahara inamalizia kazi yake na ikimaliza atafuata mapendekezo yake ya usawa wa mishahara.
-Ajira mpya atajikita kwenye kichaka cha waalimu elfu 4 ma watumishi wa afya mia kadhaa
----kupandisha mshahara NEVER Labda vyeo na madaraja maana anajua atapandisha wachache tofauti na mishahara ingehusu wafanyakazi wote
-NB
Atakwepa suala la kupunguza mishahara minono serekalini na kuongezea wenye mishahara midogo.
Suala ni wafanya kazi ila lazima achomeke Ndege, SGR, na strigle gorge

Tuendelee na utabiri........
 
kwanza itakuwa copy and paste na hotuba ya mwaka jana
atakacho sema sana ni hii kuajili walimu zaidi ya elfu NNE
atagusia takwimu za umeme kwa hasa REA III
Atagusia ujenzi wa S gorge
Atagusia ujenzi wa standard geji
Atagusia Kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma
Atagusia tume ya mishahara hivyo hawezi kuongeza mishahara kwa watumishi wasubiri ataongeza fedha nyingi kamati ikileta mapendekezo yao(makofi yataskika kwa wafanyakazi ambao sare zao ni za kijani)
 
Akijitahidi sana ni kupandisha madaraja au vyeo sio mshahara! Maana anajua vyeo atapandisha wachache tofauti na mshahara angewapandisha wote
 
Hiyo ya tatu imekaa kiukweli ukweli

Mie huyo bwana JPM nikimuongelea nahofia kupata heart attack
hahahahahahhahha.....tuchekee tu maana hakuna kingne .....huku tuki subiri tarehe ya mwisho....ya kuaga hapa dunian....
Am ignirant of th Good word in the clean Book.,Mkuu
 
Nyekundu
 
Kuna mama ataibuka na kilio kua anadai mafao sijui kadhulumiwa nn huko! JPM ataamuru alipwe!! Hapo shangwe zatatawala



Huyo mama atakuwa anahadithia huku kilio kinatawala,ataitwa muhusika wa kilio cha huyo mama ataulizwa kama anajua kuhusu malalamiko ya huyo mama
 
Halafu atapokea waunga juhudi waliokwisha andaliwa na kila mmoja ataongea kama kakaririshwa kabla... Sababu zitafanana na sifa zitakuwa kemkem
Na waliokaririshwa wasipotokea hadharani mkuu wa mkoa ajiandae
 
hahahahahahhahha.....tuchekee tu maana hakuna kingne .....huku tuki subiri tarehe ya mwisho....ya kuaga hapa dunian....

Am ignirant of th Good word in the clean Book.,Mkuu

Anakwambia maendeleo hayana chama...yule mkuu bhana

Huo mstari wa mwisho sijakuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…