Utachukulia poa au utamzingua?

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Hivi inakwaje unaenda na girlfriend kwenye show ya msanii maarufu...halafu anajipeleke jukwaani kwa kiherehere huku akimkatikia kiuno mpaka majasho huyo msanii kitu ambacho hajakufanyia.au upo na boyfriend wako halafu anaanza kumtunza huyo msanii wa kike mahela na kujipendekeza huku wakiserebuka kitu ambacho hakuwahi kukufanyia wewe?hapo wewe utafanyaje?
 
Ukiona ivo huwa hawatunzi wasanii ivo. Ujue kutunza inaweza kuwa pesa au mauno?!
 
Ukiona ivo huwa hawatunzi wasanii ivo. Ujue kutunza inaweza kuwa pesa au mauno?!
kutunza ni pesa.......ila sasa kuna mengine yanazidi
 
ina mana hujui upo na mpenz wako?

si mmeenda kustarehe? Tena muziki? Raha yake si ndo hyo? Atunze /akatike inategemea na midadi yake loh? Au akitoka pale upenzi ndo unakua umeisha?
 
mkuu mbona hujiamini...
nyie ndio mnaorushaga ngumi klabu

Hata kama jamani, viherehere vingine vimezidi!! Mtu yuko na mpenzi wake lakini ana overkiherehere, je akiwa peke yake? Sasa mtu kama huyu siku akienda peke yake, mwenzie atakuwa na amani kweli?? Well, furahi lakini muangalie na mwenzako, usimkwaze!!
 
dawa ndogo kama anamnengulia msanii na wewe kuwa msanii atakunengulia wewe badala ya mangwea. kama unaona wivu basi usiende naye, nenda peke yako
 
kazi rahisi sana, unamvuta mkono na kumwambia twende ukawakatikie na kuwatuza watoto yatima, nyambafu
 
kazi rahisi sana, unamvuta mkono na kumwambia twende ukawakatikie na kuwatuza watoto yatima, nyambafu
kama yuko na wewe halafu yuko hvo je itakwaje siku akienda mwenyewe
 
Hata kama jamani, viherehere vingine vimezidi!! Mtu yuko na mpenzi wake lakini ana overkiherehere, je akiwa peke yake? Sasa mtu kama huyu siku akienda peke yake, mwenzie atakuwa na amani kweli?? Well, furahi lakini muangalie na mwenzako, usimkwaze!!
yaani sijui akiwa mwenyewe inakwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…