Utafanya nini ugenini kama chumba unacholala kina wadudu

Utafanya nini ugenini kama chumba unacholala kina wadudu

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Kama chumba ulichotengewa upumzike ugenini kina kunguni, mende, panya nk usifanye usafi mkubwa ikiwemo kuweka dawa za kuua wadudu pia usiwaambie wenyeji kuwa hulali vizuri kutokana na adha hiyo, pasifie tu kuwa pako vizuri, itakubidi uvumilie mpaka pale utakapomaliza ugeni.
 
Ukweli utakuweka huru, kwani ukisema kutakuwa na ubaya, uzidi kuumia au kufa na tai shingoni, mi kwa upande wangu nasema tu na nafanyia usafi.
 
Kama chumba ulichotengewa upumzike ugenini kina kunguni, mende, panya nk usifanye usafi mkubwa ikiwemo kuweka dawa za kuua wadudu pia usiwaambie wenyeji kuwa hulali vizuri kutokana na adha hiyo, pasifie tu kuwa pako vizuri, itakubidi uvumilie mpaka pale utakapomaliza ugeni.
Yaan ulale na nyoka na nge chumba kimoja alafu ujichekeshe una akili wewe? Fanya usafi afya yako ni muhimu zaidi kuliko zao haijarishi watakuchukuliaje utakae ugua ni wewe sio wao
 
Mgeni kakuta mifugo ya wenyeji...😂
 
aiseee vp mbna unaandika kama unakimbizwa au ndo hao wadudu washakupanda kichwani ?????
 
Nawaambia ukweli na kuwasititiza wanifanyie usafi nilale kwa raha eboooh! Kuwaacha ni kuwaendekeza kuwa na tabia za kichawi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ilinitokea mwaka huu ..,nmeenda kwa mwenyeji wangu kwa ajili ya mualiko wa kutafuta riziki ,so ilipofika muda w kulala nililala vizuri lakini mida ya saa 8 nilistuka nikaanza kujikuna mwili mzima ile kuwasha taa tuu ya simu [emoji23][emoji23] nikakutana na askari{kunguni} kibaaao.

Kiukweli niliamka na kwenda kulala sebleni japo mwenyeji wangu na kukoloma akawa anakoloma ahahahaha.
 
Back
Top Bottom