Utafanyaje ukikumbwa na hili

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,095
Uutafanyaje endapo umeachwa na mtoto wa miaka 17 nyumbani na akaamua kusema kuwa umembaka? ni ndugu yake wa kike mkeo mtarajiwa na mkeo mtarajiwa anaamni kuwa kweli umefanya ivyo!nyumbani mliachwa wawili tuu ila nje kuna majirani .kodi ya nyumba analipa mkeo mtarajiwa na ameamua kukufukuza bila kuwa na ushaidi nawe unampenda sana mkeo je kama ni wewe imekutokea ungechukua uamuzi gani?andika ushauri au maoni yako hapa .au kama wewe ndio dada wa huyo mtoto wa kike utachukua uamuzi gani na ungalifanya nini?maana mtoto kakupigia simu kuwa alitaka kubakwa na mchumba anahajafanya hivyo
 
Uutafanyaje endapo umeachwa na mtoto wa miaka 17 nyumbani na akaamua kusema kuwa umembaka?

Alibakwa?

.....alitaka kubakwa?
 
sijui kama alibakwa au alitaka kubakwa....

Ila angejiuliza wakati anabakwa/anataka kubakwa hakupiga kelele? Majirani hawakusikia?

Tabia ya binti husika ikoje?

Tabia ya mwanaume ikoje?

Then hospitali ingehusika......
 
Duuuh, utakuwa mhalifu tu the day ulipokubali kulelewa. Zaidi kujinasua, nenda hosptal huwa kuna utafiti wakuonyesha kama umepenetrate.
 
Hpo kam mkeo mtarajiwa hakuamini ni kuchukua maamuzi magumu tu ndio njia sahihi
hakuna mtu ambaye unaye muoa halafu hakuamini siku akiambiwa umefanya kitu
kingine atakubali tu kirahisi kwani hakuamina
 
Nitawaza kuwa huo ni mpango kamambe umesukwa na mke wangu ili kuivunja ndoa yetu,na kikubwa ni kwamba mke ameshaona kuwa mimi ni mzigo na namtegemea kwa kila kitu,hivyo amechoka kufuga mbwa asiyewinda,na itanilazimu kufikiri hivyo kwasababu ya maamuzi yake ya fasta na bila kutaka kufanya uchunguzi juu ya alichokisikia!!!
 

Mgogoro upo hapo. Ningeondoka taratibu nikatafute pengineko!
 
Unawaambia kama ni kweli umembaka, basi muende hospitali mkapime na ichukuliwe PF3. Daktari watabaini kuwapo kwa chembe-chembe za manii ukeni kwa huyo binti. Huo ni ushahidi tosha, lakini uthibitisho wa DNA ni muhimu pia. Huyo binti anaweza kuwa na boifrendi wake, wametoka kujamiiana, manii yake, kisha ukaambiwa ni yako. Waambie kwa kuwa wao ndio wanaokutuhumu, wao ndio wagharamie kipimo cha DNA.

Jiamini. Kuwa na msimamo. Utamwona huyo binti akinyong'onyea na kuyeyuka kama siagi kwenye mkate (toast)!

Makosa mengi hufanyika wakati mtuhumiwa anapokuwa mwoga. Kama huna kosa, woga wa nini?

KUWA MKALI KABISA!
 
Mtandike vibao huyo mtoto halaf nenda kwenye DNA TEST
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…